in

Facebook, Apple na Makampuni Mengine 125 Kumpinga Trump

Makampuni ya teknolojia ya nchini marekani yaungana kumpinga trump

Facebook, Apple na Makampuni Mengine 125 Kumpinga Trump

Sakata zima la maswala ya uhamiaji nchini marekani linaendela wakati huu makampuni takriban 97 ya teknolojia ya nchini marekani yameamua kuungana na kupinga swala zima la raisi huyo kupinga waamiaji kutoka nchi mbalimbali.

Makampuni hayo yamefungua mashtaka kwenye mahakama ya Washington state court ili kupinga ubaguzi huo wa waamiaji kutoka nchi mbalimbali ambazo zilitajwa na rahisi huyo mapema wiki mbili zilizopita. Katika kufanya hivyo makampuni hayo yalituma Amicus briefs kwenda kwa mahakama hiyo ikitaka mahakama kufikiria shauri hilo la kuzuiwa kwa waamiaji kutoka nchi za kislamu zilizotajwa na raisi huyo.

Makampuni hayo yalio tuma nyaraka hiyo mahakamani ni pamoja na Apple, Facebook, Google, Twitter, pamoja na Microsoft, kama unataka list nzima ya makampuni hayo unaweza kudownload nakala ya nyaraka hiyo yenye ripoti hiyo pamoja na majina yote ya makampuni yanayo mpinga raisi donald trump kwenye swala hilo. Bofya hapo chini kudownload nyaraka hiyo.

Ripoti ya Makampuni.pdf

Update : Kampuni nyingine zimeongezeka na kufikia kampuni 127

Njia Mpya ya Kutengeneza Pesa Kupitia YouTube Shorts Video

Kwa habari zaidi za teknolojia usiache kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia kupata habari kwa haraka unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.