in

Tetesi Google Kununua Mtandao wa Kijamii wa Twitter

Huenda mtandao wa kijamii wa twitter ukamilikiwa na Kampuni ya Google Hivi Karibuni

google-kununua-mtandao-wa-twitter

Hivi karibuni hisa za kampuni ya Twitter zimepanda kwa takriban asilimia 20% baada ya baadhi ya ripoti kuhusu kampuni hiyo kukaribia kuuzwa kwa kampuni nyingine kubwa za teknolojia duniani iki wemo kampuni ya teknolojia ya Google.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, kampuni kubwa za teknolojia duniani zipo tayari kununua mtandao huo wa kijamii kabla ya mwisho wa mwaka huu ambapo makampuni yanayosemekana yanauwezekano mkubwa wa kununua mtandao huo ni kampuni ya Google pamoja na mtandao wa salesforce.com yakiwemo pia na makampuni mengine ambayo sio maarufu sana kwa sasa.

Hata hivyo ripoti hizo ziliendelea kusema kuwa wenyeviti pamoja na watawala wa mtandao huo wa twitter wako tayari kufunga mauzo hayo na kampuni kubwa ya teknolojia ambayo huenda ikawa ni kampuni ya Google japo kuwa hakuna ripoti kamili kuhusiana na hilo. Hata hviyo nasemekana kuwa kampuni ya twitter pamoja na mtandao huo wa kijamii vitauzwa kwa kampuni yenye bids za juu hivyo huwezekano wa kampuni ya Google kununua kampuni hiyo ni mkubwa sana.

Google imekua ikifuatilia kwa ukaribu sana mtandao wa twitter toka hapo mapema mwaka jana, bila shaka hiyo ni dalali rasmi kuwa kampuni hiyo inatamani sana kumili mtandao huo wa kijamii na huenda hivi karibuni mtandao huo ukawa chini ya kampuni hiyo maarufu ya teknolojia duniani ya Google.

Ili kujua zaidi endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Fuatilia Mpira Yote Tanzania na Duniani Kupitia Simu

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.