in

Game Bora za Programu ya Android Mwaka 2016

game bora mwaka 2016

Kama tunavyojua kucheza game kwenye smartphone yako ni kitu ambacho akikwepeki kabisa siku hizi iwe umepumzika au umeamua tu kupoteza mawazo wengi wetu ukimbilia kwenye simu zetu za mikononi ambapo kiukweli pamoja na kufanya yote ni lazima kupitia angalau kidogo kwenye game flani iliyoko  kwenye simu yako, lakini tatizo ni kwamba kuna wakati unakosa kabisa kujua ni game gani inakufaa kwenye simu yako.. maswali haya yamejibiwa leo na mkusanyiko wa game bora za programu ya android ambapo tutakusaidia kujua game bora za kipindi hichi katika simu yako… oky! twende tukaanze moja kwa moja.

Asphalt 8: Airborne

Kama wewe ni mpenzi wa game za mbio za magari game hii itakufaa sanaa kwani kwanza ina muonekano bomba na imekwepo kwa muda sana kiasi kwamba watengenezai wa game hii wanajua wanachokifanya  hivyo basi kama ungependa kupoteza muda uku uki enjoy mchezo wa mbio za magari hii game ni kwaajili yako.

Badland

BADLAND
Price: Free+

Hii ni game ambayo kwa mara ya kwanza unaweza usiione kama ni game nzuri lakini pale unapoielewa ni moja kati game zinazoweza kukufnya usiachie smartphone yako kabisa, game hii inamuonekano mzuri na ni rahisi kucheza bofya hapo juu ili uweze kuijaribu moja kwa moja.

Clash of Clans

Clash of Clans
Price: Free+

Hii inawezekana ni moja kati ya game ambazo watu wengi sana usichukulia poa lakini game hii ni moja kati ya game maarufu sana kutaoka na kuwa na uwezo mzuri wa kucheza watu wawili pamoja na vitu vingi ambavyo unaweza kuongezea kwenye game hii, game hii imeonekana sana kuteka watu wengi duniani… sasa kwanini usijaribu ili uone nini kizuri kwenye game hii. bofya hapo juu kuanza kupakua game hii moja kwa moja.

Candy Crush Saga

Candy Crush Saga
Price: Free+

Kama bado hauja cheza game hii ni moja kati ya game ambazo kwa kweli zinakufanya uone simu yako kama kitu bomba cha kupoteza muda iwe umeme umekatika alafu una game hii kwenye simu yako hakika uta enjoy sana ikiwa inapenda na watu zaidi ya 14,890,027 ni game bora na nzuri kwa wapenda game kote duniani.

Where’s My Water?

Where's My Water? 2
Price: Free+

Kama wewe ni mpenzi wa michezo ya puzzle game hii ni one of the best ukitaka kupata raha ya game kwenye simu yako hakika game hii ni sehemu nzuri sana ya kuanzia kizuri ni kwamba game hii ina matoleo matatu sasa ikiwa na maana burudani inaendelea hivyo kaa kitako na uanze kushemsha ubongo kwa game hii bomba.

Temple Run

Temple Run
Price: Free+

Kama bado haujacheza game ya temple runi itakua umepitwa sana kwani game hii ni moja kati ya game zinazo kufanya kupotelea kwenye simu yako kwani kila wakati utakapo pata nafasi lazima utakua ukuwaza gamu hii bomba game hii inaonekana kupenda sana na watu hapa tanzania.

Subway Surfers

Subway Surfers
Price: Free+

Ikiwa ni moja kati ya gemu maarufu sana tanzania na sehemu zingine game hii imeonekana kuwa na mashiko kwa watu wengi hasa kutokana na kuwa na uwezo wa kuunganisha na facebook watu wengi mbalimbali duniani wameoneka kuipenda sana game hii. ijaribu sasa bofya hapo juu kuipakua.

Angry Birds

Angry Birds Classic
Price: To be announced

Ikiwa ni game ambayo ilifanya vizuri sana kwa watumiaji wa iPhone sasa game hii ipo kwenye android na pia hivi karibuni itatoka movie ya animation inayohusu game hii kama ujaicheza game hii ninge kushauri uanze utaratibu wa kuipakua sasa hivi bofya hapo juu uanze kuipakua sasa.

Fighting Tiger – Liberal

Kwa wale wapenda game za kupigana hii ni moja kati ya game bomba sana japo kua game hii haijuilikani lakini nimeamua kuiweka kwenye list kutokana na uzuri na graphics ya game hii kama unadhani natani bofya hapo juu ipakue kisha ijaribu kwenye simu yako sasa.

Mortal Kombat X

Hii ni moja kati ya game ambayo mimi binafsi naipenda sana labda ni kwasababu nilianza kuicheza game hii toka kwenye nintendo hapo zamani..kiukweli ni kwamba gamu hii inakuja na na graphics za hali ya juu sana na pia ni moja kati ya game bora za action ijaribu sasa kisha utaniambia.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments