Kama unataka kuwasiliana na huduma kwa wateja vodacom na hutaki kusubiri kwa muda mrefu unaweza kutumia njia hii rahisi na ya haraka. Kumbuka kufuata hatua kwa hatua kama inavyoweza kuonakana hapo chini.
- Bofya namba 100 kupitia simu yako kisha bofya kitufe cha kupiga.
- Mara baada ya simu kuanza kutaja menu mbalimbali sikiliza maelezo kisha bofya namba 1 kwenye kwenye huduma nyingine za vodacom au subiri ili kuendelea. Kama maelezo ni mengi bofya 1
- Baada ya hapo sasa subiria kama sekunde moja kisha bofya namba hizi kwa mfulizo ufuatao.
- Bofya 2 (Huduma za Mpesa)
- Bofya 2 (Kama umetuma pesa Kimakosa)
- Bofya 1 (Kama umetuma kwenda kwa mitandao mingine au Bank)
- Bofya 2
- Bofya 3 (Kuwasiliana nasi kwa njia ya simu au kuongea na mtoa huduma wa Vodacom)
Kwa kutumia njia hii utaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja vodacom bila kusubiria kwa muda mrefu au kubofya namba nyingi. Kumbuka hata kama unalo tatizo lingine tumia njia hii kuwasiliana na huduma kwa wateja moja kwa moja.