March : Jaribu Apps Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Hizi hapa apps nzuri ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako sasa
March : Jaribu Apps Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android March : Jaribu Apps Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Ni muda mrefu sana umepita toka tuongelee kuhusu app nzuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android. Katika kipindi hicho nimepokea apps nyingi sana kiasi kwamba hadi sasa sijajua ni app gani niweke kutokana na kuwa bado sijaweza kufanikisha kujaribu app zote.

Kutokana na hilo leo nitaweka apps chache ambazo nimejaribu na kwa maoni yangu zinaweza kusaidia sana kwa namna moja ama nyingine. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

ActionDash

Kama wewe ni mtu ambaye una watoto au hata wewe mwenyewe ungependa kujizuia kuhusu utumiaji wako wa smartphone basi app ya ActionDash ni kwa ajili yako. App hii inaruhusu kuzuia matumizi yaliyo pitiliza ya apps mbalimbali ikiwa pamoja na kutoa ripoti za muda gani umetumia app yoyote kwenye simu yako. App hii ni rahisi kutumia na ni bora sana kama unao watoto na unataka kuzuia wasitumie app fulani kwa muda mrefu.

Advertisement

Download Hapa Action Dash

AppsFree

AppsFree
Price: Free

Kama unapenda kujaribu app mbalimbali kwenye simu yako ya mkononi ya Android basi app hii itakuwa chaguo bora sana kwako. App hii inao mkusanyiko wa apps mbalimbali ambazo zinapatikana kwenye soko la Play Store kwa kulipia lakini kupitia apps hii utazipata bure kwa muda wa kipindi maalum. App hii sio soko la apps bali inakusaidia kupata apps ambazo zipo kwenye ofa kupitia Play Store.

Download Hapa AppsFree

Tapet

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kuweka wallpaper mpya kila wakati basi unasoma makala sahihi, app hii ya Tapel inakupa uwezo wa kupata na kudownload wallpaper mpya na za kisasa kwenye simu yako kwa urahisi. App hii ni nzuri sana na inaweza kusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako kwa asilimia 100.

Download Hapa Tapel

WhatsTool

Kama wewe ni mtumiaji wa programu ya WhatsApp basi lazima utaipenda app hii, WhatsTool ni app nzuri ambayo inakusaidia kufanya maujanja mbalimbali kupitia programu ya WhatsApp. App hii itakusaidia kuona meseji alizofuta mtu kwa kupitia sehemu ya “delete for everyone”, pia utaweza kutuma meseji bila kusave namba ya mtu na mambo mengine mengi. Kama wewe ni mpenzi wa WhatsApp basi jaribu app hii na uhakika utaipenda kwa asilimia 100.

Download Hapa WhatsTool

Hermit

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hutembelea tovuti mbalimbali kwenye simu yako kila siku, basi app ya Hermet itakusaidia sana. App hii inakupa nafasi ya kubadilisha tovuti yoyote kuwa kama application. Kupitia app hii unaweza kutumia app ya Facebook bila kuinstall, instagram na mitandao mingine. Pia unaweza kuongeza tovuti nyingine na kuzitumia kama apps.

Download Hermit Hapa

StoryArt

StoryArt ni app nyingine nzuri sana kwa watumiaji wa mtandao wa Instagram, app hii inakupa uwezo wa kutengeneza video za stori au picha moja kwa moja kwa kuchagua picha kwenye simu yako. App hii inakuja na mifano mbalimbali ambayo unaweza kutumia kutengeneza storie kwa haraka na urahisi. Kifupi ni kuwa kama unataka kushangaza wafuasi wako kupitia instagram basi jaribu app hii.

Download StoryArt Hapa

Gazeti

Gazeti - Tanzania
Price: Free

Kama wewe ni mtanzania au unapenda kujua yale yote yanayo endelea nchini Tanzania basi gazeti ni app nzuri sana ya kuwa nayo.

Download Gazet Hapa

Na hizo ndio apps nzuri ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako ya Android kwa siku ya leo, kama unataka kujua apps nyingine nzuri zaidi basi hakikisha unasoma hapa kujua apps nzuri kwaajili ya kufuatilia michuano ya UEFA moja kwa moja kupitia kwenye simu yako.

Kama unayo app yako na ungependa iandikwe kupitia makala kama hizi basi unaweza kutuma jina la app yako na jinsi inavyo fanya kazi kuptia kwenye fomu ya wasiliana nasi hapo chini.

2 comments
  1. Mkuu samahani ile template ya ecommerce katika blogger upande wa kuonesha size bado inaleta shida naandika,vzur size/14 nakisha napitisha mstari katikati lakini hakuna kinacho display

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use