Zingatia Haya Kabla ya Kuwa na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Mambo kufanya kabla ya kutengeneza akaunti za mitandao ya kijamii
Zingatia Haya Kabla ya Kuwa na Akaunti za Mitandao ya Kijamii Zingatia Haya Kabla ya Kuwa na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Linapokuja swala la kuwa na akaunti za mitandao ya kijamii ni wazi kuwa kila mtu ana sababu zake.

Kuna baadhi ya watu huwa kwenye social media ili kutangaza biashara zao mbalimbali, wengine huwa kwenye social media kwa ajili ya kufurahia maisha ya kijamii pamoja na kupata habari mbalimbali.

Pamoja na hayo yote, siku ya leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kujua mambo ya muhimu ya kuzingatia kabla ya kuamua kuwa na akaunti za mitandao ya kijamii au social media.

Advertisement

Basi bila kupoteza mudam twende moja kwa moja kwenye makala hii. Kumbuka makala hii imegawanyika kwenye sehemu mbili, yaani mambo muhimu kwa mtu binafsi na mambo muhimu kwa akaunti za kibiashara.

Mambo Muhimu kwa Akaunti Binafsi

Kwa kuanza ningependa ufahamu mambo muhimu ambayo ni bora kwa mtu binafsi. Kumbuka mambo haya ni muhimu kama unataka kuanzisha Social Media kwaajili ya mambo binafsi.

Hakikisha Unatafuta Jina Sahihi

Zingatia Haya Kabla ya Kuwa na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Jina pekee linatosha kusema mengi kuhusu wewe, ni wazi kuwa ukisikia mtu anaitwa jina la ajabu ni lazima wazo litakujia kuwa kuwa mtu huyo ana tabia kama jina hilo.

Hivyo basi, jina unalo chagua ni muhimu sana liwe jina lako binafsi na kama jina lako halipatikani basi hakikisha unaweka alama nzuri kwenye jina lako.

Alama nzuri ni pamoja na underscore (_), au nukta (.), au unaweza kuchagua neno (iam), (official) au jina lolote ambalo ni bora na lenye kuonyesha utarabu au ustarabu.

Weka DP Bora Yenye Sura Yako

Zingatia Haya Kabla ya Kuwa na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Linapokuja swala la picha ni wazi kuwa watu wengi husahau nguvu ya picha. Picha ni kiungo muhimu sana na ukitumia vibaya inaweza kuharibu maisha yako.

Linapokuja swala la profile picture au DP ni muhimu kuweka picha yako yenye sura yako, hii ni muhimu hasa kama unataka kutengeneza jina lako mbele ya watu mbalimbali.

Ni wazi kuwa baadhi ya makampuni hutumia mitandao ya kijamii kuweza kujua zaidi kuhusu mtu au watu wanao waajiri. Hivyo ni muhimu sana kutumia picha nzuri yenye maadili kwenye DP yako.

Andika Bio Yenye Kueleza Kuhusu Wewe

Zingatia Haya Kabla ya Kuwa na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Moja ya sehemu ya pili ambayo mtu huangalia anapo fungua profile yako yoyote kwenye mtandao wowote wa kijamii ni pamoja na sehemu ya Bio au Biography.

Sehemu hii ni muhimu kwa kuwa ndio yenye kueleza kuhusu wewe pamoja na ukurasa wako au profile yako.

Ni muhimu kandika Bio yenye kutoa maelezo ya wewe ni nani, au unafanya nini. Hii ni muhimu kwa kuwa maelezo yako mwenyewe yanaweza kutoa picha halisi ya wewe ni mtu wa aina gani

Ni vyema kuandika bio yenye maneno mafupi ambayo inaweza kumfanya mtu ajue moja kwa moja kama wewe ni mtu wa aina gani.

Mfano unaweza kuandika “Mtanzania, muandishi wa habari wa kujitemea na mjasiriamali“.

Hii pekee inatosha kuonyesha wewe ni mtu wa aina gani na ni kutu gani ambacho ni muhimu kwenye ukurasa wako.

Weka Link Kwenye Bio

Zingatia Haya Kabla ya Kuwa na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Link kwenye bio yako ni moja ya kitu muhimu sana, hii ni muhimu kwa kuwa inaweza kusaidia kuweza kutangaza mambo ya muhimu kuhusu wewe.

Unaweza kuwaka link ya mtandao wa muhimu ambao una kazi zako zaidi. Lakini pia unaweza kuchagua kuweka link kwenye bio ambayo inaweza kuonyesha kazi zako zote ikiwa pamoja na akaunti zako za mitandao ya kijamii.

Unaweza Kutengeneza Link Kwenye Bio bure kabisa kwa kubofya hapo Hapa

Kwa kusema hayo, hayo ndio mambo ya muhimu ambayo unatakiwa kuwa kufanya kabla ya kuamua kutengeneza akaunti yoyote ya mitandao ya kijamii.

Makala inayo fuata tutaenda kuangalia mambo ya muhimu kufanya kabla ya kuwa na akaunti ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya biashara.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use