in

“Ubora wa TECNO Camon 15” Wateja Waonekana Kuipenda

TECNO Camon 15 simu inayopendwa kwa sasa nchini Tanzania

"Ubora wa TECNO Camon 15" Wateja Waonekana Kuipenda

Ikiwa ni takriban mwezi mmoja umepita tangu kampuni ya simu za mkononi ya TECNO kuzindua simu yake mpya CAMON 15 kwa njia ya mtandao, watumiaji wengi wa simu hiyo wameeleza namna simu hiyo ya CAMON 15 ilivyo na utofauti na simu za makampuni mengine na matoleo yake yaliyopita.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maduka ya TECNO kuhusu simu hiyo, watumiaji hao wamekiri kuwa CAMON 15 imekata kiu yao ya kile walichokuwa wanakihitaji siku zote kutokana na kuridhishwa na ufanisi wa mifumo endeshi ya simu hiyo pamoja na sifa nyinginezo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

"Ubora wa TECNO Camon 15" Wateja Waonekana Kuipenda

Marceline John (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya begi na msimamizi wa duka la TECNO.

“Hii simu ni moto mwingine kabisa, ni simu ambayo sijutii kununua na hapa naona pesa yangu imeenda kihalali yaani. Binafsi kinachonifurahisha sana ni mwonekano wa simu, kamera na betri” Alisema Bi. Marceline

"Ubora wa TECNO Camon 15" Wateja Waonekana Kuipenda

Bi. Shamimu Ramadhani (kushoto) na Bi. Veronica Swai (kulia) wakikabidhiwa zawadi na msimamizi wa duka la TECNO (Katikati) baada ya kununua TECNO CAMON 15.

Kwa upande wa watumiaji wengine wameelezea kuhusu CAMON 15 kuwa imewaondolea kikwazo cha kupiga picha nyakati za usiku na sasa wanaweza kupiga picha wakati wowote na mahali popote.

“Simu hii ya CAMON 15 imemaliza kabisa tatizo la kupiga picha usiku, unajua sisi wengine ni watu wa harakati nyingi sasa unapokuwa na simu kama hii picha unachukua freshi kabisa usiku na inatoka vizuri sana” Alisema Rajab Said.

"Ubora wa TECNO Camon 15" Wateja Waonekana Kuipenda
Rajab Said Mteja wa TECNO CAMON 15

TECNO ambayo ni kampuni ya simu kinara wa simu janja Tanzania imeshauza simu yake hii mpya CAMON 15 zaidi ya simu 2500 ndani ya mwezi mmoja tangu ilipozinduliwa katikati ya Aprili 2020. Mpaka sasa CAMON 15 inapatikana nchi nzima yakiwemo maduka makubwa ya TECNO na maduka ya wauzaji wa simu nchini kote

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment

  1. Nimepatwa na mashaka makubwa sana juu ya utangazaji wahizi simu za Android hususani zinazosemwa kuwa naCamera had I 4 wakati ukweli nikuwa zina kamera mmoja tu nyuma na nyingine ndogo mbele ni kwa mini mnatudanganya kiasi hicho ? simu ya CAMON 15 POUVOIR 3+ na nyingi nyinginezo zimetangazwa kwa sofa zisizo zao WHY ???,Nadhani Luna haja ya kufanya maamuzi dhidi ya Uongo huu