Tecno Yazindua Simu Mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro

Hizi hapa sifa pamoja na bei ya simu mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro
Tecno Yazindua Simu Mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro Tecno Yazindua Simu Mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro

Kampuni ya Tecno hivi karibuni imetangaza ujio wa simu zake mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro simu ambazo ni matoleo ya maboresho ya simu za Tecno Camon 11 ambazo zilizinduliwa mwaka jana 2018.

Simu hizi mpya za Camon 12 na 12 Pro hazina tofauti sana kwa sifa na Camon 11 ingawa yapo mambo ya muhimu ambayo ni tofauti kabisa kwenye simu hizi hasa toleo la Pro. Basi moja kwa moja twende tukangalie sifa pamoja na bei ya simu hizi mpya kutoka Tecno.

Advertisement

Tecno Camon 12

Tukianza na kioo Camon 12 inakuja na kioo cha inch 6.52 kioo ambacho kimetengezwa kwa teknolojia ya IPS LCD chenye uwezo wa resolution ya hadi pixel 720 x 1600. Mbali na hayo simu hii inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 16, kamera ambayo inakuja na uwezo wa kurekodi video za hadi pixel 720p@30fps, Kamera hii pia inasaidiwa na teknolojia za FaceID, HDR AI pamoja Beauty LED.

Tecno Yazindua Simu Mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro

Kwa nyuma Camon 12 inakuja na kamera tatu huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 8, kamera zote kwa ujumla zinaweza kuchukua video za hadi ya pixel 1080p@30. Kamera hizi pia zinasaidiwa na teknolojia kama vile HDR, Panorama pamoja na Face detection.

Kwa upande wa sifa za ndani Tecno Camon 12 ina endeshwa na processor ya Mediatek MT6762 Helio P22 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa hadi GB 64, kama hiyo haitoshi kwako ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory Card ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Camon 12 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Camon 12

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.52 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1600 pixels
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) na HiOS 5.5
  • Uwezo wa Processor – 4x 2.0 GHz ARM Cortex-A53, 4x 1.5 GHz ARM Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6762 Helio P22 (12 nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye teknolojia ya AI pamoja na LED Flash
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 16 nyingine inakuja na Megapixel 2 na kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 8. Kamera zote zinakuja na AI, Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Dawn Blue, Dark Jade na Sky Cyan
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, Compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor na Fingerprint.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID).

Bei ya Tecno Camon 12

Kwa sasa simu hii tayari imesha zinduliwa rasmi huko nchini Nigeria, bei yake kwa huko ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 320,000. Bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania pale simu hii itakapo zinduliwa rasmi.

Tecno Camon 12 Pro

Kwa upande wa Camon 12 Pro, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.4 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED huku kikiwa na uwezo wa kuonyesha picha za hadi resolution ya 1080 x 2340 pixels. Kwa mbele kioo hichi kina ukingo wa juu maarufu kama waterdrop notch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi sambamba kamera ya Megapixel 32 ambayo hii inauwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080p@30.

Mbali na hayo simu hii kama ilivyo Phantom 9 nayo inakuja na sehemu ya fingerprint iliyopo chini ya kioo.

Tecno Yazindua Simu Mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro

Kwa nyuma Camon 12 Pro inakuja na kamera tatu kama ilivyo kwenye Camon 12, kamera ambazo zina fanana kabisa kwa uwezo. Kamera kuu inakuja na Megapixel 16 huku kamera nyingine mbili zikiwa zina kuja na uwezo wa Megapixel 2 na Megapixel 8. Kamera zote zina uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080p@30.

Tecno Yazindua Simu Mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro

Mbali na hayo, kwa upande wa sifa za ndani Tecno Camon 12 Pro ina endeshwa na processor ya Mediatek MT6762 Helio P22 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa hadi GB 64, kama hiyo haitoshi kwako ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory Card ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Camon 12 Pro ni kama zifuatazo.

Tecno Yazindua Simu Mpya za Camon 12 na Camon 12 Pro

Sifa za Tecno Camon 12 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.39 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1600 pixels
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) na HiOS 5.5
  • Uwezo wa Processor – 4x 2.0 GHz ARM Cortex-A53, 4x 1.5 GHz ARM Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6762 Helio P22 (12 nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye teknolojia ya AI pamoja na LED Flash
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 16 nyingine inakuja na Megapixel 2 na kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 8. Kamera zote zinakuja na AI, Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3500 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Dawn Blue, Dark Jade na Sky Cyan
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, Compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor na Fingerprint.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID).

https://priceintanzania.com/comparison/tecno-camon-12-pro-vs-tecno-camon-15-pro/

Bei ya Tecno Camon 12 Pro

Kwa upande wa bei kama ilivyo Camon 12, Camon 12 Pro nayo pia inapatikana kwa sasa nchini Nigeria na bei yake kwa huko ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 390,000. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika mara baada ya simu hii kuzinduliwa rasmi hapa Tanzania.

11 comments
  1. Naitwa bahebe kidesheni.
    email yangu ni [email protected].
    Nawapongeza kwa elimu mnayotoa juu ya simu za smartphone,hii itamsaidia mnunuzi kufanya manunuzi ya simu aliyo na uelewa nayo. Hongereni sana

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use