WhatsApp Kuja na Sehemu ya Kuzuia Kuchukua Screenshot

Hutoweza kuchukua screenshot za chat zako mwenyewe ndani ya programu hiyo
WhatsApp Kuja na Sehemu ya Kuzuia Kuchukua Screenshot WhatsApp Kuja na Sehemu ya Kuzuia Kuchukua Screenshot

Hivi karibuni WhatsApp imekuwa ikifanya majaribio ya sehemu mpya ambazo zinasemekana zinakuja kubadilisha kabisa muonekano wa programu hiyo pamoja na jinsi programu hiyo inavyofanya kazi.

Moja ya sehemu hizi ni pamoja na sehemu mpya ambayo itakuwezesha kufunga programu hiyo kwa kutumia sehemu ya Fingerprint kwa simu zenye uwezo huo. Sehemu hii inamuwezesha mtumiaji kufunga programu yake ya WhatsApp kabisa hadi pale atakapoweka alama yake ya kidole ndipo aweze kuingia kwenye programu hiyo.

Lakini pia ripoti kutoka tovuti ya WABetaInfo zinadai kuwa, sehemu hiyo ya kufungua programu hiyo kwa kutumia alama za vidole itakuja sambamba na sehemu nyingine ambayo pengine watumiaji wengi wanaweza wasi ipende sana. Inasemekana kuwa pale mtumiaji anapo washa sehemu hii kupitia programu ya WhatsApp basi moja kwa moja atakuwa amewasha sehemu nyingine ambayo itakuwa ina mzuia mtumiaji kuchukua screenshot kwenye chat zake ndani ya programu hiyo.

Advertisement

WhatsApp Kuja na Sehemu ya Kuzuia Kuchukua Screenshot

Kifupi ni kuwa pale utakapo washa sehemu ya Fingerprint kwenye programu ya WhatsApp hutoweza kuchukua picha za screenshot ndani ya programu hiyo hadi hapo utakapo zima sehemu hiyo. Hata hivyo inasemekana pia baada ya kuwasha sehemu hiyo utaweza kujibu meseji kupitia sehemu ya Notification juu ya simu yako.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za chazo cha WhatsApp kuweka sehemu hii ya kuzuia mtumiaji binafsi kuchukua picha za screenshot za chat zake mwenyewe na pia bado hakuna taarifa lini sehemu hii itakuja kwenye programu za WhatsApp. Hata hivyo sehemu ya kufunga programu hiyo kwa kutumia alama za vidole tayari inapatikana kwenye simu za mfumo ya iOS.

Binafsi sioni haja ya sehemu ya kujizuia mwenyewe kuchukua screenshot ya chat zako mwenyewe hivyo sioni kama kuna maana ya sehemu hii kuwepo sambamba na sehemu ya muhimu kama ya kufungua programu hiyo kwa kutumia alama za vidole, Vipi kwako unaonaje kuhusu ujio wa sehemu hii..? tuambie mawazo yako kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use