Kampuni ya Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Xiaomi Redmi 7

Hizi hapa sifa pamoja na bei ya Xiaomi Redmi 7
Kampuni ya Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Xiaomi Redmi 7 Kampuni ya Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Xiaomi Redmi 7

Kwa sababu kampuni ya Xiaomi ina matarajio ya kuja hapa Afrika siku za karibuni, basi ni vyema ufahamu kuhusu simu zote za Xiaomi zinazotoka na zinazotarajia kutoka, sasa hivi karibuni ingizo jipya kutoka kampuni hiyo ni simu mpya ya Xiaomi Redmi 7.

Simu hii ya Xiaomi Redmi 7 ni simu ya bei nafuu na ni moja kati ya simu yenye sifa nzuri ukilinganisha na bei yake. Redmi 7 inakuja na kioo cha inch 6.26 kioo ambacho kina resolution ya 720 x 1520 pixels pamoja na teknolojia ya IPS LCD. Kioo hichi pia kinakuja na ulinzi wa Corning Gorilla Glass 5.

Kampuni ya Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Xiaomi Redmi 7

Advertisement

Kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja ya Megapixel 8 yenye uwezo wa HDR pamoja na uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 2, kamera zote za nyuma zinasaidiwa na Flash ya LED Flash.

Kwa upande wa processor Redmi 7 inakuja na processor ya Qualcomm SDM632 Snapdragon 632 (14 nm) ambayo inasaidiwa na RAM ya kuchagua kati ya GB 4, GB 3 au GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 64, GB 32 au GB 16. Sifa nyingine za Xiaomi Redmi 7 ni kama zifuatazo.

Sifa za Xiaomi Redmi 7

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.26 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×1.8 GHz Kryo 250 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 250 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM632 Snapdragon 632 (14 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 506.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu tatu moja ikiwa na GB 64, GB 32 na nyingine GB 16..
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu tatu moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 3 na nyingine ikiwa na GB 2.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0, HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.2, 1.25µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 ambayo ni depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0 Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Blue, Black na Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Xiaomi Redmi 7

Kwa upande wa bei, Xiaomi redmi 7 inakuja kwa bei tofauti kulingana na ukubwa wa ndani. Simu yenye RAM ya GB 2 na ukubwa wa GB, itauzwa kwa Yuan CNY 699 ambayo ni sawa na TSh 250,000 bila kodi. Simu yenye RAM GB 3 na ukubwa wa GB 32, itauzwa kwa Yuan CNY 799 ambayo ni sawa na Tsh 280,000 bila kodi. Simu yenye RAM ya GB 4 na ukubwa wa GB 64 itauzwa kwa Yuan ambayo ni sawa na Tsh 350,000 bila kodi. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kwa hapa Tanzania. .

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use