in

Huawei Yazindua Simu Mpya za Huawei P30 na Huawei P30 Pro

Hizi hapa sifa kamili pamoja na bei ya Huawei P30 na Huawei P30 Pro

Huawei Yazindua Simu Mpya za Huawei P30 na Huawei P30 Pro

Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye hivi leo kampuni ya Huawei imezindua simu zake mpya za Huawei P30 pamoja na Huawei P30 Pro, Simu hizi mwaka huu zimekuja zikiwa zimeboreshwa sana zaidi hata ya simu za mwaka jana za Huawei P20 na P20 Pro, pia zaidi ya simu mpya za Samsung Galaxy S10 na S10 Plus.

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Samsung najua sasa umetaka kusoma zaidi ili kujua ni kitu gani ambacho ni bora kwenye simu hizi kuliko simu mpya za Galaxy S10, kujua zaidi endelea kusoma makala hizi nitakwabia baadae kuhusu hilo. Baada ya kusema hayo hebu twende tukangalia sifa za simu hizi mpya za Huawei P30 na P30 Pro.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Huawei P30

Tukianza na simu ya Huawei P30 kama ilivyokuwa kwenye tetesi simu hii inakuja na kioo cha inch 6.1 chenye resolution ya 1080 x 2340 pixels, huku kikiwa na kime tengenezwa kwa teknolojia ya OLED. Kwa mbele simu hii inakuja na ukingo wa juu mdogo, ambao unatumika kuhifadhi kamera ya mbele ambayo hii inakuja na uwezo wa Megapixel 32. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu ambazo zina Megapixel 40 (ambayo hii ni wide lens), Megapixel 16 (ultrawide) na Megapixel 6 ambayo ni (telephoto).

Huawei Yazindua Simu Mpya za Huawei P30 na Huawei P30 Pro

Simu hii pia inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi, hivyo imepewa alama ya IP53. Lakini mbali na hayo P30 inakuja na processor ya HiSilicon Kirin 980 (7 nm) ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8 pamoja na ukubwa wa ROM wa kati ya GB 64, GB 128, na GB 256. Ukubwa huu unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory card ya Nano Memory, yenye uwezo wa hadi GB 256. Mbali na hayo sifa nyingine za Huawei P30 ni kama hizi zifuatazo.

Huawei Yazindua Simu Mpya za Huawei P30 na Huawei P30 Pro

Sifa za Huawei P30

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.1 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.6 GHz Cortex-A76 & 2×1.92 GHz Cortex-A76 & 4×1.8 GHz Cortex-A55).
  • Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 980 (7 nm).
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP10.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu simu yenye GB 64, GB 128 na GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye f/2.0, HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 40 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/1.7″, PDAF/Laser AF na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.2, 17mm (ultrawide), PDAF/Laser AF na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 8 ambayo ni f/2.4, 80mm (telephoto), 1/4″, 3x optical zoom, PDAF/Laser AF, OIS. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya dual-LED dual-tone.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3650 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 5.0, A2DP, aptX HD, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tano za Aurora, Amber Sunrise, Breathing Crystal, Black na Pearl White.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi IP53.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, color spectrum.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Huawei P30

Kwa upande wa bei, Huawei P30 inapatikana kwa pre-order kuanzia leo kwa euro €800 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 2,114,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128. Kumbuka bei hii inaweza kupanda kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha.

Huawei P30 Pro

Kwa upande wa Huawei P30 Pro hapa ndio ningependa wale wapenzi wa Galaxy S10 hapa muwe makini. Huawei P30 Pro inakuja na sifa nzuri sana ikiwa pamoja na kioo kikubwa cha inch 6.47 chenye resolution ya 1080 x 2340 pixels, ambacho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya OLED. Mbali na hayo P30 Pro inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 32.

Kwa nyuma Huawei P30 Pro inakuja na kamera nne ambazo hizi zinakuja na Megapixel 40 ambayo ni wide lens, Megapixel 20 ambayo ni ultra wide lens, na Megapixel 8 ambayo ni Periscope telephoto lens. Vilevile kamera ya nne ni TOF 3D camera.

Sasa hapa kwenye upande wa kamera Huawei P30 Pro inakuja na kamera yenye uwezo ambao hakuna simu yoyote yenye uwezo huo. Kamera ya Megapixel 8 ambayo ni Periscope telephoto lens, hii inakuja na uwezo mkubwa wa ku-zoom hadi mara 30 zaidi. Hivyo basi kama wewe ni mpenzi wa kamera basi simu hii ya Huawei P30 Pro ni simu  ya kuwa nayo mwaka huu 2019.

Kama umefanikiwa kuangalia video hapo juu najua utakuwa umejua mengi kuhusu simu hii mpya ya Huawei P30 Pro, kama unataka kujua kwa ufupi kuhusu processor, simu hii nayo inakuja na processor ya HiSilicon Kirin 980 (7 nm) ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 8 au GB 6, vilevile simu hii inakuja na ukubwa wa ROM wa kati ya GB 128, GB 256 na GB 512. Simu hii pia inaweza kuongezewa na memory card ya Nano Memory, yenye uwezo wa hadi GB 256. Mbali na hayo sifa nyingine za Huawei P30 Pro ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei P30 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.47 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.6 GHz Cortex-A76 & 2×1.92 GHz Cortex-A76 & 4×1.8 GHz Cortex-A55).
  • Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 980 (7 nm).
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP10.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu simu yenye GB 128, GB 256 na GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye f/2.0, HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 40 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/1.7″, PDAF/Laser AF na nyingine ikiwa na Megapixel 20 yenye f/2.2, 16mm (ultrawide), 1/2.7″, PDAF na kamera nyingine inakuja na Megapixel 8 ambayo hii ni Periscope yenye, f/3.4, 125mm (telephoto), 1/4″, 5x optical zoom, OIS, PDAF, kamera ya mwisho ikiwa ni TOF 3D camera. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya dual-LED dual-tone.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4200 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging. Inakuja na uwezo wa kuchaji simu nyingine kwa Wifi
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 5.0, A2DP, aptX HD, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tano za Aurora, Amber Sunrise, Breathing Crystal, Black, Pearl White
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi IP68.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, color spectrum.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Huawei P30 Pro

Kwa upande wa bei Huawei P30 Pro inapatikana kwa pre-order kuanzia siku ya leo kwa euro €1,000 ambayo ni sawa na Tsh 2,640,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 8 na ukubwa wa ndani wa GB 128. Toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 256 itauzwa kwa Euro €1,100 ambayo ni sawa na Tsh 2,905,000 bila kodi. Toleo la mwisho lenye GB 512 itauzwa kwa Euro €1,250 ambayo ni sawa na Tsh 3,300,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kuongezeka kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha.

Na hizo ndio sifa pamoja na bei ya Huawei P30 na P30 Pro, kama umefanikiwa kusoma hadi hapa ningependa kujua maoni yako unaonaje simu hizi je ni bora kuliko simu za Galaxy S10 na S10 Plus..? Tumabie kwenye maoni hapo chini.

Huawei Yazindua Simu Mpya za Huawei P30 na Huawei P30 Pro
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments

  1. Kwenye camera inawezekana kamzidi samsung ila kwenye proceser na gpu hatufahamu tofauti ya mali na adreno na hzo namba zake ipi inanguvu zaidi ningependa utuletee makala itakayo fafanua hivi vitu.