in

Simu Zenye Kutoa Kiasi Kikubwa cha Miozi (SAR) Mwaka 2019

Pia soma hapa kujua simu zenye kutoa kiasi kidogo cha miozi au SAR

Simu Zenye Kutoa Kiasi Kikubwa cha Miozi (SAR) Mwaka 2019

Kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi lazima utakuwa unajua angalau kidogo kuhusu miozi inayotolewa na simu, Kama kwa namna yoyote ulikuwa hujui kuhusu hili basi unaweza kusoma zaidi hapa ili kujua jinsi ya kuangalia kiasi cha miozi kinacho tolewa na simu yako.

Sasa kwa mujibu wa tovuti ya cancer.org, baadhi ya miozi hiyo inayotolewa na simu inaweza kusababisha matatizo ya kiafya ikiwa pamoja na uvimbe kichwani. Sababu hii na nyingine nyingi ndio zimefanya leo nikuletee list ya simu mpya za mwaka 2019 zenye kutoa kiasi kikubwa cha miozi, ikiwa pamoja na list ya simu ambazo pia zinatoa kiasi kidogo cha miozi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kama ulisoma makala yetu iliyopita, utaweza kujua kila simu inakuja na Specific Absorption Rate au (SAR), SAR ni kipimo ambacho kinatumika kupima kiasi cha miozi inayotolewa na simu yako, kadri kiwango cha (SAR) kinacho tolewa na simu yako kinavyozidi kuwa kikubwa ndivyo uwezekano wa kupata matatizo ya kiafya unavyozidi kuwa mkubwa,

Kwa mujibu wa tovuti ya Statista, hapo chini utaweza kuona list ya simu za mwaka 2019 zenye kutoa kiwango kikubwa cha SAR huku simu yenye kutoa kiwango kikubwa zaidi ikiwa ni Xiaomi Mi A1 ambayo inatoa kiasi cha 1.75 (SAR).

Simu Zenye Kutoa Kiasi Kikubwa cha Miozi (SAR) Mwaka 2019

Kwa watumiaji wa Simu za Samsung Galaxy Note 8 hapa hauna haja ya kuwa na wasi wasi kwani kwenye list inayofuata ya simu zenye kutoa kiasi kidogo cha miozi, Galaxy Note 8 imeshikila namba moja kwenye list ya simu zenye kutoa kiasi kidogo cha miozi.

Simu Zenye Kutoa Kiasi Kikubwa cha Miozi (SAR) Mwaka 2019

Na hiyo ndio list ya simu zenye kutoa kiwango kikubwa na kidogo cha miozi ambayo inaweza kuleta madhara kwenye afya yako. Kwa sasa kama simu yako ipo kwenye list ya simu zenye kutoa miozi kwa wingi, unachotakiwa kufanya ni kutumia simu yako kwa uangalifu hasa pale unapo ongea na simu jaribu kutumia headphone hasa kama unaongea na simu kwa muda mrefu.

Pia hakikisha usitumie simu yako sana hasa pale inapo pata moto kwani wakati huo ndio kiasi kikubwa cha miozi kinazalishwa zaidi, kujua zaidi hakikisha unasoma makala niliyokwambia hapo juu itakusaidia kujua zaidi jinsi ya kujilinda.

Jinsi ya Kutumia Google Bard, Mfumo wa AI Kama ChatGPT

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

6 Comments

      • tukubali tu ukweli mchungu kuwa jamii ya simu za Tecno, Infinix n.k ni simu duni zenye sura nzuri. Ni ufisadi tu wa serikali zote za Africa zimeamua kuwaruhusu wenye hizi kampuni kuwaibia wananchi wao. hizi simu zitatuletea maradhi ya cancer huko mbeleni na haiwezekani na haiingii akilini simu za kutoka China ziuzwe Africa wakati huko China hizo simu haziuzwi na hazipatikani popote.