FB Messenger, WhatsApp na Instagram Kuunganishwa Pamoja

Mitandao hii itakuwa na mwingiliano wa pamoja
mitandao ya kijamii kuunganishwa mitandao ya kijamii kuunganishwa

Hivi karibuni kumekuwa na ripoti kuhusu ku-unganishwa kwa mitandao ya kuchat ya Facebook Messenger, WhatsApp pamoja na Instagram. Kwa mujibu wa ripoti kutoka GSMArena, muungano huo unategemewa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu 2019, au mwanzoni mwa mwaka 2020.

Hata hivyo inasemekana kuwa Apps zote za mitandao hiyo zitaendelea kufanya kazi kwa kujitegemea kama kawaida, lakini inasemakana kutakuwa na aina mpya ya mwingiliano baina ya app hizo.

FB Messenger, WhatsApp na Instagram Kuunganishwa Pamoja

Advertisement

Kwa sasa bado haijajulikana jinsi gani mitandao hiyo itakavyofanya kazi pale itakapo unganishwa, ila kuna tetesi zinasema kuwa kutakuwa na mwingiliano wa meseji kupitia mitandao hiyo ijapokuwa hakuna uhakika sana kwenye hilo.

Kwa mujibu wa GSMArena, chanzo cha kufanya muungano huo ni kueleta urahisi wa kutumia huduma za Facebook pamoja na kuongeza ulinzi zaidi hasa ule wa end-to-end encryption ambao unapatikana zaidi kwenye programu za WhatsApp pamoja na Facebook Messenger.

Kwa sasa muungano unajulikana ni ule ambao, kama unatumia tovuti ya Facebook kwenye kompyuta au kama unatumia app ya Facebook page manager, utaweza kuona meseji na Comment za page yako ya FB pamoja na Instagram, na pia utakuwa na uwezo wa kuzijibu meseji kutoka kwenye mitandao yote ya FB messenger na Instagram moja kwa moja kupitia ukurasa wako wa Facebook wa kibiashara.

Kwa upande wa WhatsApp bado hakuna sehemu yoyote yenye muunganisho wa programu hiyo zaidi ya Sehemu ya matangazo, pamoja na post kwenye kurasa ya kibiashara ya Facebook ambapo unaweza kuweka namba yako na mtu ataweza kuwasiliana na wewe moja kwa moja kwa kubofya namba chini ya post husika.

Ni wazi kuwa muungano huu utaleta mabadiliko makubwa kwenye programu hizi na pengine hizi ni hatua za awali za mtandao wa Facebook kuleta matangazo kwenye App ya WhatsApp kama ilivyo tangazwa hapo awali.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use