in

M-Pesa Kenya Yaja na (Overdraft) Tumia Pesa Zaidi ya Ulizonazo

Sasa utaweza kutoa kutumia Pesa zaidi ya ulizonazo kwenye akaunti yako

m-pesa kenya overdrafts

M-Pesa ni moja kati ya huduma za kifedha zinazotumika sana Afrika Mashariki, Pia Vodacom kupitia M-pesa imekuwa ikifanya ubunifu mpya kila siku kuhakikisha watumiaji wa huduma zake wanapata kile wanacho hitaji.

Siku za karibuni tulisikia kuhusu huduma mpya ya M-Pesa Mastercard ambayo inakuwezesha kufanya manunuzi mtandaoni kwa kutumia akaunti ya M-Pesa, huduma hii kwa sasa imesaidia watu wengi sana Afrika Mashariki kuweza kufanya manunuzi mtandaoni kwa urahisi hasa kwa watu ambao walikuwa hawana akaunti za benki.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Lakini kama haitoshi hivi karibuni M-Pesa kupitia Safaricom ya Kenya imeanzisha huduma mpya ya Overdraft. Hii ni huduma mpya ambayo inawawezesha wateja wa M-Pesa kutumia pesa zaidi ya zile walizonazo kwenye akaunti zao. Kwa mfano kama ulikuwa unataka kununua kitu cha Ksh 10,000 na kwenye akaunti yako ya M-Pesa unayo Ksh 8,000, basi unaweza kununua kitu hicho na M-Pesa itakuwekea Overdraft ya Ksh 2,000 ambayo itakuja kukatwa baadae utakapo weka hela kwenye akaunti yako.

Kwa mujibu wa tovuti ya The East African, huduma hii itakuwa inawezekana kama ukiwa unatumia huduma za M-Pesa kulipia kitu unachotaka kununua. Huduma hiyo mpya iliyopewa jina la Fuliza, itakupa uwezo wa kuweka deni au Overdraft hadi ya Shilingi za Kenya Ksh 50,000 ambayo ni takribani zaidi ya Tsh 1,000,000.

Huduma hii imewezeshwa kwa ushirikiano wa kampuni ya Safaricom ya nchini Kenya pamoja na benki ya Kenya Commercial Bank (KCB) pamoja na Commercial Bank of Africa (CBA).

Kwa sasa bado hakuna taarifa kuhusu huduma hii kuja hapa nchini Tanzania, lakini kwa sababu benk hizo zinafanya kazi pia hapa Tanzania, pengine siku sio nyingi unaweza kusikia kuhusu huduma hii hapa Tanzania.

Kuhakikisha unakuwa wa kwanza kupata habari huduma hii itakapo kuja endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

M-Pesa Kenya Yaja na (Overdraft) Tumia Pesa Zaidi ya Ulizonazo
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.