Mambo 5 Ambayo Ulikuwa Hujui Kuhusu Kampuni ya Google

Yafahamu mambo haya matano makubwa kuhusu kampuni ya Google
Je Wajua Google Je Wajua Google

Ni jumapili nyingine tunakutana tena kwenye makala hizi za Je Wajua na leo nimekuandalia mambo matano ambayo inawezekana ulikuwa huyajui kuhusu kampuni maarufu ya Google.

Google ni moja kati ya kampuni zenye historia kubwa sana, ukizingatia ni moja kati ya kampuni zinazotoa huduma za kuunganisha watu kwa kutumia internet kuliko kampuni nyingine hii ni kutokana na Google kuwa na huduma nyingi sana zinazotumiwa na mamilioni ya watu.

  • Jina Google linatokana na neno la kihisabati

Pengine ulishawahi kujiuliza kwanini nini jina Google.? basi kifupi ni kuwa aliyegundua jina Google alikuwa ni mwana mahesabu kwani jina Google linatokana na neno la kihesabu “googol” neno hili maana yake ni 1 na sifuri 100.

Advertisement

  • Mwanzo Google ilikuwa inaitwa “Backrub”

Hapo mwaka 1996 wagunduzi kutoka chuo cha Stanford cha nchini marekani Sergey Brin na Lary Page walianza kufanyia kazi project yao ya kwanza ambayo ilikuwa inahusu mambo ya tovuti na jina la project hiyo lilikuwa Backrub, jina ambalo baadae lilibadilishwa na kuitwa Google.

  • Google hukodisha Mbuzi kwaajili ya Kukata Majani nje ya Ofisi zake

Pengine unge hisi kwa kuwa Google ni kampuni tajiri sana basi lazima kuna watu wa kutunza na kukuta majani ya kwenye Garden za nje ya ofisi yake lakini, Kama sehemu ya kutunza mazingira, kampuni ya Google hutumia wanyama mbuzi kukata majani nje ya ofisi zake.

  • Google ilikua inahifadhiwa kwenye Hard Disk yenye ukubwa wa GB 4

Hapo zamani GB 1 ilikua ikionekana kama ndio memory kubwa sana kiasi kwamba huduma zote za Google pamoja na Tovuti yake ilikuwa ikihifadhiwa kwenye Server yenye ukubwa wa GB 4, Kingine cha kushangaza ni kuwa Server hiyo ilikuwa imetengenezwa kwa toi za kuchezea watoto maarufu kama LEGO.

  • Google ina miliki kikoa hichi “466453.com” sababu ndio hizi

Google ina miliki vikoa (domain) kadhaa ambazo zimekosewa lakini zina maana ya Google, kwa mfano google inamiliki vikoa vilivyokosewa vya Gooogle.com, Gogle.com, Googlr.com zote zikiwa kwa matamshi zina maana ya neno Google. Kuhusu kikoa cha 466453.com google ina miliki kikoa hichi kutokana na namba hizo kwenye keyboard ya simu yako ya tochi zina maana ya neno “Google”.

Na hayo ndio mambo ambayo nimekuandalia leo kuhusu kampuni ya Google, nini maoni yako je unaonaje historia nzima ya Google pamoja na mambo haya niliyokuandalia leo..? tuambie maoni yako hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use