in

Samsung Yagawa Bure Simu Zake Mpya za Galaxy Note 8

Wasafiri wa ndege kutoka nchi ya Spain wapewa simu zaidi ya 200

Samsung Yagawa Note 8

Samsung Note 8 ni simu ambayo iko kwenye gumzo kubwa sana duniani kote, kwa hapa Tanzania simu hii ina thamani ya takribani shilingi milioni 2, lakini kama haitoshi simu hii pia imeonekana kuwa na sifa bora pengine kuliko simu zote za samsung mpaka sasa.

Katika kuongezea gumzo, siku ya jana wasafiri wa ndege kutoka nchi ya Spain waliokuwa wanatoka Madrid kwenda A Coruna walifaidika na simu za Galaxy Note 8 zilizokuwa zinagaiwa buree kabisa na kampuni ya Samsung ndani ya ndege hiyo.

Samsung iligawa simu zake hizo bure kwa lengo la kuwa hakikishia wateja wake wa nchini humo kuwa simu zake kwa sasa ni salama kabisa kusafiri nazo kwenye ndege. Kampuni hiyo ilitoa bure simu zaidi ya 200 ambazo zilikuwa na ujumbe uliokuwa ukisomeka “A year ago we asked you to turn it off, we welcome you today on board.”

Ujumbe huo ulikuwa ukimaanisha kuwa mwaka jana kampuni hiyo iliomba wateja wa simu zake za Note 7 wasipande nazo kwenye ndege kutokana na simu hizo kulipuka, lakini mwaka huu kampuni hiyo imerudi na kuwahakikishia wateja wake kuwa simu hizo sasa ni salama kabisa hata kwenye ndege.

Kampuni ya Airtel ya Kwanza Kuja na eSIM Tanzania

Je nini maoni yako kuhusu hili..? tuandikie kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia usisahau kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store nasi tutakujuza habari zote za teknolojia kwa haraka zaid

Chanzo : Tech Cruch

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments