in

Programu Bora Zinazoweza Kukusaidia Kwenye Afya Yako

Programu hizi ni bora sana kwa upande wa Afya yako ya kila siku

Programu za Afya

Ukweli ni kwamba kuna programu nyingi sana kwenye masoko ya Google Play Store pamoja na App Store na kama usipokuwa na muda utakuta huwezi kujua programu ambazo pengine kwa namna moja au nyingine zingekusaidia kwenye maisha yako ya kila siku, ndio maana leo Tanzania Tech tunakuletea programu hizi ambazo zitakusaidia sana kwenye swala zima la afya..Oky leeets go..

9. Google Fit – Fitness Tracking

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

App hii inasaidia sana kwenye swala zima la kuangalia ni kiasi gani umetembea au muekimbia au kama unataka kukumbushwa kila wakati wa kufanya mazoezi unapofika au wakati wa kunywa maji basi app hii ni bora sana na ina mambo mengi sana ambayo yanaweza kukusaidia afya yako kuwa bora kwa kutumia simu yako ya mkononi.

8. Pharmacy – Generic Medicines

App hii ni bora sana hasa kwenye swala zima la dawa, kwa kutumia app hii utaweza kujua mambo mbalimbali kuhusu dawa kabla hauja amua kununua dawa hizo. App hii inauwezo wa kukupa habari kuhusu dawa yoyote huku ikikuonyesha na mathara ya dawa hiyo au kwa kitaalamu Side Effect, kifupi ni kwamba app hii ni bora sana kuwa nayo ili kujua vizuri kuhusu dawa tunazotumia kila siku.

7. Home Remedies+ : Natural Cures

Kwa wale wanaopenda kujitibu kwa kutumia tiba za asili basi app hi ni bora sana, app hii inauwezo wa kukupa maelekezo ya kufanya tiba za asili ambazo zinaweza kukusaidia kutibu magonjwa mbalimbali kwa haraka, yote hayo unaweza kuyapata kupitia simu yako ya mkononi.

6. Disorder & Diseases Dictionary

Ukweli ni kwamba app hi ni muhimu sana kuwa nayo kwenye simu yako kwani app hii itakusaidia kujua dalili mbalimbali moja kwa moja kwenye simu yako, kama unataka kujua kuhusu chochote ambacho kimekua kikikusumbua kwa muda mrefu basi app hii inaweza kukusaidia sana kutambua dalili hizo.

5. Period Tracker, My Calendar

App hii ni moja kati ya app ambazo zinatumiwa sana na wadada wengi sana ili kujua tarehe za mwezi au hedhi, app hii inasaidia watu wengi sana na sidhani kama kuna mdada ambaye hana app hii, kama huna basi download sasa uweze kujua kuhusu siku zako za hatari.

4. WebMD Baby

WebMD Baby
Price: Free

App hii ni moja kati ya app tano bora kwenye list hii, app hii ni muhimu sana kwani itakusaidia wewe kama baba au mama au kama unatarajiwa kuwa hivyo hivi karibuni. App hii itakusai kujua mabo muhimu kama vile jinsi ya kufunga nepi, ni chakula gani kinaitajika kwa mtoto wa umri gani, kujua ni muda gani mtoto anastaili kulala au chakula gani anatakiwa kula na mengine mengi.

3. Medscape

Medscape
Price: Free

Medscape ni moja kati ya app ambazo ni bora sana, app hii inaweza kusaidia watu wenye taaluma mbalimbali ikiwa pamoja na watumiaji wa kawaida. App hii inauwezo wa kusaidia watu wanaojifunza udakitari ikiwa pamoja na madaktari pia app hii inaweza kuwasaidia watu wa kawaida au wagonjwa kwa kujua dalili za magonjwa pamoja na tiba ambazo zitaweza kukusaidia. kifupi app hii ni bora sana na inasaidia sana hivyo nakushauri ni vyema kuwa nayo kwenye simu yako.

2. WebMD for Android

Hii ni moja kati ya app ambazo ni bora sana yani sana, app hii itakusaidia kujua kuhusu magonjwa mbalimbali kwa kugusa sehemu inayo uma kwenye wa mtu ulioko kwenye app hiyo yaani kama unaumwa kichwa kwenye app hii kuna picha ya mtu hapo utagusa kichwa na utaulizwa mambo kuhusu kichwa chako kama kinauma au vipi. Mwisho ni kwamba aoo hii ni moja kati ya app bora sana na nakushauri kama bado huna app hi basi download sasa.

1. Your.MD: Health Care Assistant

Mwisho kabisa kwenye namba moja ni app hii ya YourMD app hii ni moja kati ya app bora sana kwani utahisi kama unaongea na daktari kwani app hii inakupa nafasi ya kuchat na app hii ili kuweza kujua matatizo yako mbalimbali, kwa mfano kama unataka kujua dalili za ktu flani unaweza kuuliza app hii kwa kuandika dalili ulizo nazo na app hii itakuuliza maswali ambayo kutokana na majibu yako basi app hii itakwambia unasumbuliwa na nini huku ikikushauri kuchukua hatua mbalimbali za kitabibu. App hii ni bora sana na ni moja kati ya programu bora sana za afya kwenye soko la Play Store na pengine.

Na hizo ndio programu ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukusaidia wewe kuweza kujua mambo mbalimbali kuhusu afya yako. Kama una maoni au maswali yoyote usisite kutuandikia maoni yako hapo chini nasi tutashulika kukujibu moja kwa moja…

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Amani Joseph

Programu Bora Zinazoweza Kukusaidia Kwenye Afya Yako

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Nzuri Kwaajili ya Kupakua Video za Aina Yoyote

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.