in

Facebook Kuongeza Sehemu Mpya ya Kutafuta na Kuomba Kazi

Mtandao wa facebook unazidi kuwa mtandao bora zaidi

Kazi Facebook

Wote tunajua ugumu ulipo katika swala zima la kutafuta ajira, ndio mana Facebook kupitia mtandao wake wa facebook sasa inakuja na sehemu mpya ya kukuruhusu wewe kutafuta mfanya kazi au kuomba kazi.

Sehemu hiyo mpya itasaidia wale wenye page za kibiashara za facebook (Business Pages) kutuma list ya nafasi za kazi kwenye kurasa zao hizo huku wale wanao penda (like) page hiyo wakipata uwezo wa kupenda (kulike), kutoa maoni (kucomment) pamoja na kuomba (kuapply) kazi moja kwa moja kwenye kurasa hizo bila kutoka nje ya mtandao wa facebook.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa sasa sehemu hiyo mpya inategemewa kutoka leo kwenye nchi za US pamoja na Canada, kwa tanzania bado haijatangazwa sehemu hii inakuja lini ila ni vizuri kukumbuka kuwa sehemu hiyo itakuja kwa wale wenye kurasa za kibiashara pekee hivyo kabla sehemu hiyo haijaja Tanzania hakikisha page yako ni ya kibiashara ili uweze kupokea sehemu hiyo.

Kwa taarifa kamili kuhusu sehemu hiyo itakuja lini Tanzania endelea kutembelea Tanzania tech kila siku au unaweza kupakua App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa wakati, pia unaweza kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia youtube kama unataka kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Facebook Kuongeza Sehemu Mpya ya Kutafuta na Kuomba Kazi
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.