Programu 5 Mpya za Android za Kiswahili Mwezi 8 (2016)

Hizi ni Baadhi ya Programu Mpya za Android Kuingia kwenye Play Store
Programu mpya za Android Kiswahili Programu mpya za Android Kiswahili

Kila siku hapa tanzania pamoja na nchi zingine jirani kasi ya kutaka kujua kuhusu teknolojia inaongezaka kwa kasi sana hivyo pia teknolojia nayo imeonekana iki-itajika kwa kasi sana, ndio mana hata watanzania pamoja na makampuni mbalimbali yameonekana kuleta programu nyingi mabalimbali mpya zenye kusaidia mambo mbalimbali kuanzia habari, michezo na hata kwenye swala zima la teknolojia kwa ujumla.

Hivyo basi hizi ni baadhi ya programu mpya za kiswahili ambazo tanzania tech imefanikiwa kuziona kutoka kwenye soko la Play Store.

Bongo Leo

Advertisement

Bongo Leo
Price: Free

Hii ni programu iliyotengenezwa na kampuni ya Green Telecom Limited, programu hii inakusaidia kupata habari kutoka kwenye blog mbalimbali za habari hapa nchini tanzania ikiwemo Bongo 5 millard ayo na blog nyingine kubwa za habari hapa nchini, pia programu hiyo inakusaidia kutuma habari zako pale utakapokua umezipata.

Ajira Yako

Programu 5 Mpya za Android za Kiswahili Mwezi 8 (2016)
The app was not found in the store. 🙁

Kwa kutumia programu hii iliyotengenezwa na Jr Media  utakua na uwezo wa kupata kujua nafasi mpya za kazi mbalimbali za hapa nchini tanzania pamoja na kupata taarifa pindi tu ajira mpya inapowekwa kwenye programu hiyo mpya ya ajira hapa tanzania.

Tanzania Tech

Hii ni programu iliyotengenezwa na kampuni ya digital webbase na ni programu inayokusaidia kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako na kwa haraka zaidi.

Mtoko

Mtoko
Price: To be announced

Hii ni programu iliyotngenezwa na Bahari Technologies Ltd programu hii inakusaidia kupata kujua sehemu zipi mbalimbali za kwenda ili kubadilisha mazingira na kustarehe ikiwa pamoja na kujua ratiba za sinema na mengineyo.

Le Mutuz Blog

Le Mutuz Blog
Price: Free

Hii ni programu iliyotengenezwa na One Point Network, programu hii inahusu habari zote zinazotoka kwenye blog ya williammalecela.com.

Hizi ni baadhi tu! ya programu ambazo tumefanikiwa kuziona kwenye soko la Play Store, kama wewe ni mwandishi wa programu au hata unataka tu programu yako iandikwe kwenye blog ya tanzania tech tafadhali Wasiliana nasi na utupe maoni yako, pia unaweza kupata habari za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use