Editor choice

#Uchambuzi : Kwa nini Ununue au Usinunue Galaxy M21

Karibia wiki nzima sasa nimekua nikitumia simu ya Samsung Galaxy M21 ambayo hadi sasa naandika makala hii bado natumia simu hii ambayo nimeipata kwaajili ya majaribio.

Kupitia makala hii nitakuelezea maoni yangu kuhusu simu hii ikiwa pamoja na mambo ambayo nimegundua kuhusu simu hii mpya ya Samsung ambayo imezinduliwa mwaka 2020 mwezi wa tatu. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Samsung Galaxy M21

#Uchambuzi : Kwa nini Ununue au Usinunue Galaxy M21
TZS 820,000
Version: Unofficial Specifications
Brand: Samsung
Category: Simu Mpya
Linganisha
 • CPU: Octa-core (4x2.3 GHz Cortex-A73 & 4x1.7 GHz Cortex-A53)
 • RAM: 4/6 GB
 • Storage: 64/128 GB
 • Display: Super AMOLED, 6.4 inches
 • Camera: Triple 48 MP, 8 MP, 5 MP
 • OS: Android 10.0

Maoni Yetu

Maoni yetu baada ya kuchambua simu

7.5 3.8 119
 • Muundo 7 / 10
 • Kamera 8 / 10
 • Uwezo 7 / 10
 • Chaji 8 / 10

Soma Zaidi Hapa

Muonekano wa Galaxy M21

Tukianza na muonekano Galaxy M21 imetengenezwa kwa plastik kwa nyuma na mbele ina kioo cha inch 6.5 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED, kioo hicho pia kinakuja na uwezo wa nits hadi 420 nits (typ). Mbali na yote Galaxy M21 inakuja na ulinzi wa kioo wa kioo cha Corning Gorilla Glass 3.

Kwa upande wangu sifa zote hizo ni nzuri lakini kitu kimoja sikupenda kuhusu muonekano wa mbele wa simu hii. Galaxy M21 inakuja na kioo chenye mkato wa water drop notch, muonekano huu unafanana kwenye simu nyingi sana za Samsung, iwe ni Galaxy M31, M21s au simu yoyote ambayo ipo kwenye kundi hili la simu.

Kufanana huku kunafanya simu hii kuonekana ya kawaida sana bila kujali thamani ya simu hii. Samsung wamefanikiwa kutengeneza simu nzuri lakini pengine muonekano huu wa mbele ungetakiwa kubadilika hasa pale unapo nunua toleo la mbele la simu hii kama vile Galaxy M31s. Hivyo kama unataka kununua simu hii hakikisha kuwa haujalishi kufanana na watu wengine kwani simu hii inafanana sana na simu nyingi za sasa.

Uwezo wa Galaxy M21

Kwa upande wa uwezo wa simu hii ya Galaxy M21 hapa kuna mengi sana ya kuzungumzia, kwa kuwa ni mengi nitaongelea tu sehemu ambayo naona ni tatizo kwenye simu hii. Kwa ujumla Galaxy M21 ni simu nzuri kwa uwezo, lakini pia inategemea na toleo unalotumia, Galaxy M21 inakuja kwa matoleo mawili toleo la ROM ya GB 64 na RAM ya GB 4, pamoja na toleo la ROM ya GB 128 na RAM ya GB 6.

#Uchambuzi : Kwa nini Ununue au Usinunue Galaxy M21 1

Kama wewe ni mtu ambaye unatumia sana simu kwenye vitu kama Games na kutumia app nzito sana kama vile geekbench na nyingine kama hizo basi hakikisha una nunua toleo la GB 128 na RAM GB 6. Binafsi nimefanikiwa kufanya majaribio ya simu zote mbili na Galaxy M21 yenye GB 64 na RAM 4 inaonekana kama kwenye Games haifanyi vizuri sana kama toleo lenye GB 128 na RAM 6.

Hivyo kama unataka kufanya zaidi na simu hii basi hakikisa unajiongeza zaidi kwa kununua toleo la GB 128 kwani utaweza kufanya mengi bila kuwa na wasi wasi wa kutumia muda mrefu. Mbali na hayo kama wewe ni mtu wa kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii na kutumia app kama Tanzania tech basi simu hii ni bora sana kwako.

Uwezo wa Kamera za Galaxy M21

Kwa upande wa uwezo wa kamera, Galaxy M21 ni simu nzuri japokuwa sio chaguo bora sana. Kwa muda wote ambao nimekuwa na simu hii nimejaribu kupiga picha mbalimbali na ukweli ni kuwa simu hii inapiga picha vizuri lakini rangi ya picha mara nyingi imekuwa ikitofautiana sana na simu yangu ya Galaxy C7 Pro ambayo nimekuwa nikitumia kwa miaka 3 sasa.

image

Galaxy M21 inakuja na kamera tatu kwa nyuma, kamera kuu ikiwa na Megapixe 48, kama wewe ni mtu ambaye unanunua simu kwa kuangalia namba basi pengine ni vyema kujua kuwa kuna wakati “ukubwa wa pua sio wingi wa makasi”.  Kifupi binafsi nahisi kuwa uwezo wa software ya kamera ya simu hii bado sio bora sana kwani kuna wakati simu hii haiwezi kurekebisha rangi vizuri. Labda Samsung wanaweza kubadilisha hili kwa ku-update app ya kamera.

Software ya kamera ni kitu cha muhimu sana ili kuweza kufanya picha iwe bora bila kujali idadi ya Megapixel kwenye kamera. Google Pixel na iPhone ni moja ya simu ambazo hutumia zaidi Software kuliko ukubwa wa pixel kwenye kamera, hii ndio maana simu hizi zinaweza kuchukua picha vizuri sana pengine kuliko simu nyingi sana za sasa. Hivyo kwa kusema hayo ni vyema nikwambie kuwa kamera ya Galaxy M21 ni bora lakini usitegemee maajabu.

Uwezo wa Battery Galaxy M21

Hapa naomba nisikuandikie maneno mengi sana kwani tayari utakuwa unajua kuwa simu hii inakuja na uwezo mkubwa sana wa kudumu na chaji. Simu hii ipo kwenye list ya simu zenye battery kubwa ya 6000 mAh, hivyo ni wazi kuwa simu hii inaweza kudumu na chaji kwa muda mrefu.

#Uchambuzi : Kwa nini Ununue au Usinunue Galaxy M21 2

Wakati wa majaribio yangu nimeweza kukaa na simu hii bila kuchaji ndani ya siku nzima huku nikiwa nimetumia kwa mutumizi makubwa kama vie kucheza game, kusikiiza muziki, social media kidogo pamoja na kuperuzi kwa sana. Simu hii ina uwezo wa kudumu na chaji siku nzima bila wasi wasi na baada ya siku kuisha unaweza kubakiwa na chaji hadi asilimia 40 au 30.

Kifupi kama wewe sio mtu wa atumizi makubwa basi unaweza kukaa na simu hii kwa siku mbili bila kuchaji na bila kuwa na wasi wasi hata kidogo. Kitu pekee ambacho ni tatizo kwa upande wangu ni kuwa simu hii inatumia muda mrefu sana kujaa chaji hadi asilimia 100, mimi mara nyingi hutumia lisaa limoja au masaa mawili kujaa hadi asilimia 100. Hili ni moja kati ya tatizo la kuwa na battery kubwa ni wazi kuwa lazima ichukue muda kujaa.

Mengineyo

Hapa labda nikwambie kuwa Galaxy M21 ni simu ngumu lakini sio ngumu sana kwani kama unavyojua simu hii imetengenezwa kwa plastik, pia kioo chake ni kigumu lakini sio sana kwani ni Gorilla Glass 3 na sio 5 hivyo hakikisha unaweka protector kwani inaweza kukusaidia angalau kidogo.

Pia ni vyema ufahamu kuwa processor ya simu hii sio processor bora sana kwani bado haina nguvu kubwa ya kuendesha games kubwa kubwa kama PUBG ikiwa kwenye resolution kubwa. Pia app kubwa sana zinaweza kuwa zina kwama kwama kidogo. Kumbuka matoleo yote ya GB 64 na GB 128 yanakuja na processor ya aina moja, ila toleo la GB 128 ilinaweza kufanya kazi bora zaidi kwenye Games kwa sababu ya ongezeko la RAM ya GB 6.

Hitimisho

Baada ya kusema hayo yote sasa moja kwa moja haya hapa ndio maoni yangu kwanini ununue au usinunue simu mpya ya Galaxy M21.

5.9 Total Score
Kwa nini ununue au Usinunue Galaxy M21

Baada ya kukaa na simu hii kwa muda wa wiki moja nimegundua kuwa kama unataka simu yenye uwezo wa kudumu na chaji na yenye kufaa kwa matumizi ya kawaida ya kila siku basi nunua Galaxy M21.

6.6Expert Score
Muonekano wa Galaxy M21
5
Uwezo wa Galaxy M21
7
Uwezo wa Kamera za Galaxy M21
6.5
Uwezo wa Battery Galaxy M21
8
5.2User's score
Muonekano wa Galaxy M21
1
Uwezo wa Galaxy M21
5
Uwezo wa Kamera za Galaxy M21
8
Uwezo wa Battery Galaxy M21
7
PROS
 • Galaxy M21 inadumu na chaji sana.
 • Galaxy M21 ina uwezo mkubwa.
 • Galaxy M21 ina toleo la Android 11.
CONS
 • Galaxy M21 haina kamera bora sana.
 • Muonekano wa Kufanana
 • Imetengenezwa kwa Plastiki

Tanzania Tech
Logo