in

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Hakuna mtu ambaye ataweza kuiba picha yako kwa namna yoyote ile

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Katika ulimwengu wa sasa wa mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook na mitandao mingine ni wazi kuwa picha zina thamani kubwa sana, iwe wewe ni mtu binafsi, mfanyabiashara au wewe ni mwandishi wa habari ni wazi kuwa picha inaweza kukusaidia kubadilisha maisha kwa namna moja ama nyingine.

Kuliona hilo hivi leo nimekuletea njia rahisi na fupi ambayo inaweza kukusaidia kuweka kuzuia picha zako kuibiwa kwa kuweka alama kwenye picha zako ili kuweza kukusaidia kuweza kupata haki miliki na kutaarifu watu kuwa picha inatoka kwako.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Najua utakuwa unawaza kuwa njia hii ni kama njia nyingine ambazo mtu anaweka username kwenye picha, lakini njia hii ni tofauti kwani utaweza kuweka alama au watermark kwa namna ambayo hakuna mtu yoyote ambae anaweza kuondoa. Pia unaweza kuweka picha (logo) au maandishi kwenye picha yako.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, hiyo ni namna moja ambayo unaweza kuweka watermark kwenye picha yako kwa urahisi na haraka. Basi moja kwa moja twende kwenye hatua hizi rahisi.

Kwa kuanza unaweza kupakua app kupitia link hapo chini, app hii, app hii kuipata ni bure kabisa unaweza kutumia bila matangazo ya aina yoyote.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii na kuinstall kwenye simu yako moja kwa moja sasa endelea kwenye, kwa kufungua app hii kisha chagua picha unayotaka kuweka watermark, hakikisha picha hiyo ipo kwenye simu yako.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Baada ya kuchagua picha moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa kuweka watermark ambao ndio utatumia kubadilisha muonekano ikiwa pamoja na mambo mengine mbalimbali.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Baada ya kuingia kwenye ukurasa huo moja kwa moja bofya sehemu ya Content iliyopo sehemu ya chini upande wa kulia.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Kupitia sehemu hii ndipo utakapo chagua aina ya Watermark unayo hitaji, unaweza kuchagua watermark ya picha au logo kwa kubofya Icon, au unaweza kuchagua maandishi kwa kubofya sehemu ya Text.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Baada ya kuchagua moja kati ya hizo sasa utapeweza kuchagua Style, kama unatumia watermark ya maandishi au kama umechagua sehemu ya Text kwenye hatua iliyopita basi utaweza kuweka Emoji na maandishi mengine, pia kupitia sehemu hii ya Style utaweza kubadilisha rangi ya maandishi ikiwa pamoja na njia ya kufanya maandishi hayo yakolee zaidi au yafifie, unaweza kubadilisha yote kwa kuchagua sehemu ya Style kisha chagua Alpha. Pia utaweza kubadilisha Angle kwa kuchagua sehemu ya Angle iliyopo chini ya Alpha.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Baada ya hapo sasa unaweza kubofya sehemu ya Layout ambapo hapa ndipo unapoweza kuchagua aina ya Muundo wa watermark unayo hitaji. Unaweza kuchagua watermark iliyo jaa kwenye picha au kuchagua watermark ndogo ndogo lakini zikiwa kwenye kioo kizima kwa mfano wa picha ya kwanza kabisa kwenye ukurasa huu.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Unaweza kubadilisha muonekano wa kuchagua huku ukisogeza sehemu ya Horizontal pamoja na Vertical, kadri unavyo sogeza kwa kuongeza au kupunguza ndipo unapo ona muundo wa watermark kwenye picha ukibadilika. Unaweza kuona kwenye picha hapo chini.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Baada ya hapo kama utaridhika na matokeo basi moja kwa moja unaweza kusave picha yako kwenye Gallery ya simu yako kwa kubofya sehemu ya kusave ndani ya App hiyo.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Baada ya hapo moja kwa moja utakuwa umeweza kuweka watermark kwenye picha yako, kwa urahisi na haraka.

Uzuri wa kutumia app hii ni kuwa, baada ya kuandika maandishi au kuchagua logo unayotaka ionekana kwenye picha zako, huna haja tena ya kuchagua logo kila wakati bali sasa kila utakapo chagua picha kwa ajili ya kuweka watermark utakuwa huna haja ya kufanya hatua hizi kwenye kila picha au kuchagua logo au maandishi kila wakati.

Kitu pekee ambacho unaweza kuitaji kufanya ni kuchagua rangi inayo endana na picha na pia kubadilisha position au Angle kulingana na muundo wa picha. Unaweza kupata sehemu hiyo kupitia sehemu ya Style kama nilivyo onyesha kwenye picha hapo juu.

Hadi hapo natumaini maujanja haya yanaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kudownload nyimbo yoyote ya audio na video kupitia simu yako ya Android.

Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kufuta Kwa Haraka Picha na Mafaili Yanayofanana

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments