Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Pia utaweza kuweka muda ambao barua pepe hiyo itajifuta yenyewe
Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Katika ulimwengu huu wa sasa ni wazi kuwa kila mmoja wetu anahitaji usiri kwa namna moja ama nyingine. Kuliona hili siku ya leo nimekuletea njia rahisi ambayo itakusaidia kutumia email ya siri moja kwa moja kwa kutumia mtandao wa Gmail.

Njia hii ni bora kama unataka kutumia mtandao wa Gmail kuweza kutuma ujumbe wa barua pepe za siri kama vile ripoti mbalimbali za siri za ofisi na mambo mengine kama hayo. Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye hatua hizi.

Kwa kuanza fungua gmail kwenye akaunti yako, kama unatumia kompyuta kama mimi basi moja kwa moja andika gmail.com au andika google.com/gmail na utapelekwa moja kwa moja kwenye barua pepe yako ya gmail.

Advertisement

Baada ya hapo bofya kitufe cha Compose ilia kuanza kuandka email au barua pepe yako.

Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Baada ya hapo andika kila kitu unachotaka na hakikisha umekamilisha kila kitu kwenye barua pepe yako. Hakikisha kila kitu kimeandikwa kwa usahihi.

Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Baada ya kumaliza kuandika kila kitu, moja kwa moja bofya kitufe cha kufuli kilichopo chini karibia na kalamu mwisho kabiasa wa uwanja wa kuandika barua pepe.

Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Baada ya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye uwanja ambapo unatakiwa kuandika muda ambao barua pepe yako itaisha muda wake, chagua muda huo kisha moja kwa moja chagua sehemu ya SMS passcode kisha bofya Save.

Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Ukisha maliza kila kitu sasa endelea kwa kubofya Send, Baada ya hapo utaweza kuletewa sehemu ya kuweka namba ya simu ya mtu unae mtumia barua pepe hiyo, hii ni muhimu kwani mtu huyo atapokea password ambayo ndio atatumia kuweza kufungua barua pepe hiyo.

Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Chagua namba ya nchi yako uliyopo kwa kubofya bendera, kisha andika namba ya mpokeaji na kisha bofya Send. Baada ya hapo mpokeaji atapokea barua pepe hiyo ambayo itakuwa na kitufe cha Send passcode ambapo kwa kubofya kitufe hicho ataweza kujitumia password ambayo ndio atatumia kuweza kufungua barua pepe hiyo.

Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Mpokeaji ataweza kuweka password na aliyopokea kwenye sehemu ambayo itatokea mara baada ya kubofya sehemu ya Send passcode.

Jinsi ya Kutuma Barua Pepe ya Siri Kupitia Google Gmail

Kwa kufanya hatua hizo moja kwa moja utaweza kutuma barua pepe ya siri kwa kutumia mtandao wa Gmail. Kumbuka unaweza kujitumia passcode hizo bila kukatwa gharama yoyote kwenye simu yako.

Kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupata barua pepe ya kazi mtu yoyote kwa urahisi na haraka. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use