in

Samsung Yazindua Simu ya Bei Nafuu ya Galaxy M01

Simu nyingine ya bei nafuu kutoka kampuni ya Samsung

Samsung Yazindua Simu ya Bei Nafuu ya Galaxy M01

Kampuni ya samsung hivi leo imetangaza toleo jipya la simu ya bei rahisi ya Galaxy M01, simu hii inafuatia muendelezo wa simu za bei nafuu ambazo kampuni ya Samsung iliahidi kuzikutoa zaidi hapo mwaka 2018.

Simu hii ya Galaxy M01 ni toleo ambalo linafanana kidogo na toleo la Galaxy A01, simu nyingine ya bei rahisi ambayo ilitoka rasmi mwezi wa pili mwaka huu 2020.

Kwa upande wa simu mpya ya Galaxy M01, simu hii inakuja na kioo cha inch 5.71 kioo ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya PLS TFT. Kioo hicho pia kinakuja na uwezo wa kuonyesha picha na video zenye resolution ya hadi pixel 720 kwa 1560.

Samsung Yazindua Simu ya Bei Nafuu ya Galaxy M01

Tukiwa bado upande wa mbele, Galaxy M01 inakuja na kamera ya mbele ya megapixel 5 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video zenye resolution ya hadi pixel [email protected]

Kwa upande wa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili, kamera kuu inakuja na Megapixel 13 huku kamera nyingine ikiwa na Megapixel 2. Kamera zote kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video zenye resolution ya hadi [email protected]

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Kwa upande wa sifa za ndani, Galaxy M01 inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 439 (12 nm), processor ambayo ina speed ya CPU ya hadi Octa-core (4×1.95 GHz Cortex-A53 & 4×1.45 GHz Cortex A53). CPU hiyo inapewa nguvu na RAM ya GB 3 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 32. Unaweza kuongeza uhifadhi huo kwa kutumia memory card yenye hadi GB 256.

Kwa upande wa battery, Galaxy M01 inakuja na battery kubwa ya 4000 mAh battery ambayo inaweza kudumu na chaji hadi siku moja nzima kulingana na matumizi yako. Simu hii inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama (headphone jack), huku pia ikiwa na Radio FM.

Unaweza kusoma Hapa Kujua Bei ya Galaxy M01

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.