Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 4 na Pixel 4 XL

Kwa upande wa sifa Simu hizi hazi tofauti kubwa sana na simu za mwaka jana
Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 4 na Pixel 4 XL Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 4 na Pixel 4 XL

Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye leo kampuni ya Google imatangaza toleo la nne la simu zake mpya za Google Pixel. Google Pixel 4 na Pixel 4 XL ni matoleo mpya ya simu hizo ambazo zinakuja na maboresho kadhaa ukilinganisha na simu za Google Pixel za mwaka jana 2018.

Kwa kuanza, Google Pixel 4 inakuja na kioo cha inch 5.7 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya OLED chenye uwezo wa kuonyesha picha na video zenye resolution hadi ya pixel 1080 x 2280. Tofauti na simu nyingine za Pixel zilizo tangulia, simu hii ya Google Pixel 4 haina ukingo mkubwa wa juu bali inakuja na kioo kilicho jaa kwa asilimia kubwa.

https://youtu.be/_F7YRde8DuE

Advertisement

Kwa upande wa kamera, Pixel 4 inakuja na kamera mbili za nyuma, huku kamera kuu ikiwa inakuja na megapixel 12 na nyingine ikiwa na megapixel 16. Kamera hizi zinasaidiwa na teknolojia mbalimbali kutoka Google ikiwa pamoja na teknolojia za Auto-HDR, na panorama huku zikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera mbili kamera moja ikiwa na megapixel 8 na kamera nyingine ikiwa ni TOF 3D camera.

Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 4 na Pixel 4 XLKwa upande wa sifa za ndani, Pixel 4 ina endeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 855 inayo saidiwa na CPU yenye uwezo wa hadi Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.78 GHz Kryo 485), inayo saidiwa na RAM ya hadi GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 64 na GB 128. Sifa nyingine za Google Pixel 4 ni kama zifuatazo.

Sifa za Google Pixel 4

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.7 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~444 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.78 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 845 (10 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 64 na nyingine inakuja na GB 128 zote zikiwa Hazina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili kwa mbele, moja ikiwa na uwezo wa Megapixel 8 moja ikiwa na f/1.8, 28mm (wide), PDAF na nyingine ikiwa ni TOF 3D Camera no AF.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.7, 28mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, dual pixel PDAF, OIS, na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.4, 45mm (telephoto), 1.0µm, PDAF, OIS, 2x optical zoom. Kamera zote zinasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 2800 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1 Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Clearly White, Just Black, na Oh So Orange .
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM lakini pia unaweza kutumia eSim (laini ya simu inayo unganishwa koja kwa moja na kampuni ya simu na sio ile ya kadi), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi IP68 (inakaa kwa dakika 30 kwenye maji yenye urefu wa mita 1.5).
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint bali inakuja na ulinzi wa kutambua uso (Face ID).

Bei ya Google Pixel 4

Kwa mujibu wa Google, Google pixel 4 inategemewa kupatikana hivi karibuni kwa dollar za marekani $800 ambayo ni sawa na shilingi za tanzania TZS 1,841,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka kwa hapa Tanzania.

Kwa upande wa Google Pixel 4 XL, hakuna kitu cha tofauti sana na Google Pixel 4 zaidi ya ukubwa wa kioo, pamoja na ukubwa wa battery. Sifa nyingine za Pixel 4 XL zinafanana kabisa na Pixel 4. Unaweza kusoma sifa za Pixel 4 XL hapo chini.

Google Yazindua Simu Mpya za Google Pixel 4 na Pixel 4 XL

Sifa za Google Pixel 4 XL

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3040 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~537 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.78 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 845 (10 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 64 na nyingine inakuja na GB 128 zote zikiwa Hazina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili kwa mbele, moja ikiwa na uwezo wa Megapixel 8 moja ikiwa na f/1.8, 28mm (wide), PDAF na nyingine ikiwa ni TOF 3D Camera no AF.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.7, 28mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, dual pixel PDAF, OIS, na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.4, 45mm (telephoto), 1.0µm, PDAF, OIS, 2x optical zoom. Kamera zote zinasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3700 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1 Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Clearly White, Just Black, na Oh So Orange .
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM lakini pia unaweza kutumia eSim (laini ya simu inayo unganishwa koja kwa moja na kampuni ya simu na sio ile ya kadi), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi IP68 (inakaa kwa dakika 30 kwenye maji yenye urefu wa mita 1.5).
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint bali inakuja na ulinzi wa kutambua uso (Face ID).

Bei ya Google Pixel 4 XL

Kwa upande wa bei ya Pixel 4 XL, Simu hii inategemewa kuingia sokoni hivi karibuni kwa dollar za marekani $900 sawa na shilingi za kitanzania TZS 2,070,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kuongezeka kwa hapa nchini Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use