in

Kampuni Yalipa Tsh Bilioni 4.2 Kwa Kumtag Kim Kardashian Instagram

Mbali na Bilioni 4.2 pia kampuni hiyo inatakiwa kulipa Zaidi ya Milioni 100 za Wakili

Kampuni Yalipa Tsh Bilioni 4.2 Kwa Kumtag Kim Kardashian Instagram

Kama wewe umekuwa mtumiaji wa mtandao wa Instagram ni wazi unajua kuwa kwa sasa instagram imekuwa ni chanzo kikubwa cha mapato kwa wasanii, pamoja na watu wengi maarufu. Sio kitu cha ajabu kuona makampuni makubwa yakifanya biashara za mamilioni na wasanii au watu maarufu na kupata faida kubwa.

Kwa sababu Instagram imekuwa ni chanzo kikubwa cha mapato, wasanii na watu maarufu sasa wamekuwa makini na brand zao na kama ukifanya mchezo na brand ya mtu basi unaweza kufungwa au kutozwa faini ya mamilioni ya pesa kwa kosa ambalo pengine ungeona kama kitu cha kawaida kama vile kutag akaunti ya mtu bila idhini yake.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sasa kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, Kim Kardashian West ambae ni mke wa msanii, mwigizaji, mjasiriamali na mtayarishaji wa muziki Kanye West, ameshinda kesi ambayo alifungua kwa kushtaki kampuni moja ya nchini marekani inayojihusisha na mambo ya Fashon kwa kosa la kutag akaunti yake ya Instagram mara kwa mara bila idhini yake.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Inasemekana kuwa kampuni hiyo inayotumia jina la Missguided kwenye mtandao wa Instagram, imekuwa na tabia ya kuweka nguo zinazo fanana na nguo anazo vaa Kim Kardashian na hivyo kufanya watu wanunue nguo hizo wakizani kampuni hiyo ina ushirikiano na mwana mitindo hiyo. Hata hivyo inasemekana kuwa, kampuni hiyo imekuwa ikitumia sehemu ya promotion inayo onekana kwa juu kwenye picha ya Instagram, kuonyesha ushirikiano wa kampuni hiyo na Kim wakati kukiwa hakuna ushirikiano wowote uliokwepo kati ya kampuni hiyo na mwana mitindo hiyo

Kampuni Yalipa Tsh Bilioni 4.2 Kwa Kumtag Kim Kardashian Instagram

Mbali na faini hiyo ya bilioni 4.2 ambazo kampuni hiyo imetakiwa kulipa, pia imetakiwa kulipa kiasi kingine cha dollar za marekani $59,600 ambayo ni sawa na takribani Tsh Milioni 137, hii ikiwa ni malipo ya mwanasheria wa mwanamitindo huyo. Vile vile Kim ameitaka kampuni hiyo kuacha kabisa kutumia akaunti yake kwa namna yoyote ya kimauzo, matangazo au kibiashara.

Kwa sasa kampuni hiyo imeshafuta picha zote ambazo zilikuwa na muonekano wa Kim pamoja na kufuta Tag zote ambazo zilikuwa kwenye picha za matangazo mbalimbali ya nguo na bidhaa nyingine.

Kim Kardashian ni Moja ya watu 20 wanaolipwa pesa nyingi zaidi kupost Tangazo kwenye mtandao wa Instagram, akiwa analipwa zaidi ya Bilioni 1 kwa kupost Tangazo moja kwenye akaunti yake ya Instagram. Hata hivyo hiyo ni kwa mwaka jana 2018 hivyo mwaka huu lazima gharama zake zimepanda, unaweza kusoma list kamili hapa.

Kampuni Yalipa Tsh Bilioni 4.2 Kwa Kumtag Kim Kardashian Instagram
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.