in

Apps Nzuri za Kusaidia Kufuatilia Michuano ya AFCON 2019

Utaweza kuangalia mpira Mubashara pamoja na kupata matokea kwa urahisi

Apps Nzuri za Kusaidia Kufuatilia Michuano ya AFCON 2019

Kama wewe ni mpenzi wa mchezo wa mpira wa miguu basi ni wazi unajua kuwa michuano ya AFCON 2019 au Africa Cup of Nations inatarajiwa kuanza rasmi hapo kesho tarehe 21. Sasa kutokana na kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zinashiriki kwenye michuano hiyo, ni wazi ungependa kujua yote yatakayojiri kwenye michuano hiyo inayo fanyika rasmi huko nchini Misri.

Kupitia makala hii nitaenda kushare na wewe apps nzuri za Android na iOS ambazo zitakusaidia kuweza kufuatilia michuano hiyo ya AFCON 2019 moja kwa moja kupitia simu yako. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie apps hizi.

SuperSport

SuperSport
Price: Free
‎SuperSport
Price: Free

SuperSport ni moja kati ya channel ambazo zimefanikiwa kununua leseni ya kuonyesha michuano hiyo hapa Tanzania pamoja na Afrika mashariki, hivyo basi kama unataka kujua yote ya muhimu kuhusu michuano ya AFCON 2019 ni wazi kuwa unahitaji kuwa na apps za SuperSport. Unaweza kupakua apps hizo za Android na iOS hapa juu.

Live Africa Cup 2019 (CAN 2019)

Hii ni app mpya kabisa ya Android ambayo inakuja na channel mbalimbali ndani yake ambazo zinategemewa kuonyesha michuano ya AFCON 2019, kupitia app hiyo utaweza kuangalia channel mbalimbali za michezo na utaweza kuangalia kwa haraka sana bila kukata kata.

Apps Nzuri za Kujaribu Kwenye Simu Yako ya Android

Live scores for the African Cup 2019

Kama unataka kufuatilia michuano ya AFCON 2019 kwa kujua data zote za muhimu basi ni vyema kupakua app hii, app hii itakupa uwezo wa kujua magroup ya timu yalivyo pangwa utaweza kujua mechi inayochezwa siku hiyo pamoja na muda kwa saa za mahali ulipo, pia utaweza kujua viwanja vya mpira vitakavyo tumika pamoja na historia za timu na nchi mbalimbali.

LiveScore

LiveScore pia ni app ambayo inaweza kukupa matokeo na habari mbalimbali za ligi mbalimbali ikiwa pamoja na AFCON 2019, Tofauti ya app hii na nyingine ni kuwa utaweza kupata habari na matokeo pamoja na video fupi, kifupi ni kuwa app hii inajulikana sana na sidhani kama kuna haja ya kuelezea sana app hii.

All Football

All Football pia ni app nyingine ambayo inajulikana sana, app hii itakusaidia kufuatilia michuano ya AFCON 2019 kwa urahisi kwa kupata habari mbalimbali kuhusu muchuano hiyo pamoja na matokeo ya mechi mbalimbali. Unaweza kupakua app hii kwenye mfumo yote ya Android pamoja na iOS.

Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia

Goal Live Scores

GOAL Live Scores
Price: Free
‎Goal Live Scores
Price: Free

Goal Live Scores ni app nyingine nzuri ambayo itakuweka kaburibu na michuano ya AFCON 2019, app hii nayo ni ya siku nyingi na kama wewe ni mpenzi wa mpira wa miguu basi najua lazima unayo app hii kwenye simu yako kama ulikuwa ume uninstall basi ni wakati wa kuinstall app hii tena. Unaweza kuipata kwenye mifumo yote ya Android na iOS.

Kwa sasa hizo ndio baadhi ya apps ambazo unaweza kutumia kuangalia michuano ya AFCON 2019, kama unataka kujua zaidi kuhusu apps nyingine nzuri basi unaweza kusoma hapa kwenye makala yetu iliyopita. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia kama unataka kujua apps nzuri kwa vitendo basi hakikisha una subscribe channel yetu ya Tanzania Tech hapa.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.