in

Zifahamu kwa Undani Hizi Hapa Sifa na Bei ya Motorola One Vision

Simu hii ni bora pengine kuliko simu nyingine za Motorola zilizotoka hivi karibuni

Zifahamu kwa Undani Hizi Hapa Sifa na Bei ya Motorola One Vision

Kampuni ya Motorola hapo jana imezindua simu mpya ya Motorola One Vision, simu hii ni ya kisasa kabisa na inakuja na sifa nzuri sana ukilinganisha na simu nyingine za motorola zilizotoka hivi karibuni.

Motorola One Vision inakuja na na kioo cha inch 6.3 chenye resolution ya 1080 x 2520 pixels ambacho pia kimetengezwa kwa teknolojia ya FHD+ IPS LCD ambacho pia kwa juu kina ulinzi wa Corning Gorilla Glass. Kioo hicho kwa mbele kina hifadhi kamera ya selfie ya Megapixel 25 ambayo inaweza kurekodi video hadi za hadi pixel [email protected]

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili, kamera moja ikiwa na Megapixel 48 huku kamera ya nyingine ikiwa na Megapixel 5. Kamera zote za nyuma zinasaidiwa na flash mbili za LED ambazo zitasaidia kuweza kupiga picha vizuri kwenye mwanga hafifu kwa kushirikiana na teknolojia ya AI.

Mbali na hayo, Motorola One Vision inaendeshwa na processor ya Exynos 9609 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 128, ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory card ya MicroSD yenye ukubwa wa hadi GB 512. Sifa nyingine za Motorola One Vision ni kama zifuatazo.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

TABLE OF CONTENTS

Sifa za Motorola One Vision

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.3 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2520 pixels, pamoja na uwiano wa 21:9 ratio (~432 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.2 GHz
 • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9609.
 • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP3.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa memory card ya hadi GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – GB 4
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye f/2.0, 0.9µm.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.7, 1/2″, 0.8µm, PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash za Dual-LED dual-tone.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 35000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, BDS, GALILEO, SBAS. USB 3.1 ya Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Bronze gradient na Sapphire gradient.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Zifahamu kwa Undani Hizi Hapa Sifa na Bei ya Motorola One Vision

Bei ya Motorola One Vision

Kwa mujibu wa blog ya Motorola, Motorola One Vision inapatikana hivi sasa kwa nchini Brazil, huku kwa nchini Europe simu hii ikitegemewa kuingia sokoni siku ya leo, kwa Euro €300 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania Tsh 773,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka kwa Tanzania.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.