in

Video : Angalia Ugumu na Ubora wa Simu ya OnePlus 7 Pro

Kama unataka kununua simu hii soma kwanza makala hii

Video : Angalia Ugumu na Ubora wa Simu ya OnePlus 7 Pro

Kampuni ya OnePlus hapo jana ilizindua simu mpya za OnePlus 7 na OnePlus 7 Pro, simu hizi zinakuja zikiwa na ubora wa hali ya juu huku zikiwa na maboresho makubwa sana tofauti na simu za mwaka jana (2017) za OnePlus 6.

Sasa baada ya simu hizi kuweza kuzinduliwa rasmi, tayari tumefanikiwa kuona majaribio mbalimbali ya kuangalia ugumu na ubora wa simu mpya ya OnePlus 7 Pro. Majaribio hayo mengi yanalenga upande wa ugumu wa kioo pamoja na ugumu wa kamera ya mbele ambayo inatumia mota maalum kuweza kuingia au kutoka pale mtu anapotaka kuitumia.

Kwa kuanza labda tuangalie wote kwa pamoja ugumu na ubora wa simu hiyo kwa ujumla ikiwa pamoja na ugumu wa simu hiyo kwa nyuma, kwa mbele kwenye kioo pamoja na ubora wa simu hiyo pale inapokunjwa kwa nguvu.

Baada ya kuangalia ubora wa simu hiyo kwa ujumla sasa tuangalie ugumu na ubora wa kamera ya mbele ambayo inatumia Moto maalum, Kampuni ya OnePlus inadai kuwa kamera hiyo ya mbele ni ngumu sana kiasi cha kuweza kubeba tofali pale inapokuwa imechomoza kama unavyoweza kuona kwenye video hapo chini.

Dalili za Ugonjwa wa Kupenda Smartphone Kupita Kiasi

Kama unavyoweza kuona simu ya OnePlus 7 Pro ni simu ngumu sana na ukweli ni moja kati ya simu nzuri sana kuwa nayo kwa mwaka huu 2019. Kama unataka kujua zaidi kuhusu tofauti iliyopo kati ya simu hizi mbili yaani OnePlus 7 Pro na OnePlus 7, unaweza kusoma hapa.

Written by Jackline John

Jack ni mpenzi wa teknolojia napenda kuandika kuhusu maujanja, simu na kompyuta. Unaweza kunipa maujanja kupitia [email protected]

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment