in

Ripoti : Samsung Yaongoza Kwenye List ya Simu Zinazo Nakiliwa Zaidi

Kampuni ya samsung imeongoza kwa kuwa na simu feki ikifatiwa na Apple

Ripoti : Samsung Yaongoza Kwenye List ya Simu Zinazo Nakiliwa Zaidi

Kunakili au ku-copy simu ni moja ya kati ya vitu ambavyo vimezoeleka sana hasa kwa siku hizi. Kudhibitisha hilo hivi karibuni, ripoti kutoka kwa watafiti wakubwa wa masoko ya simu za mkononiĀ AnTuTu imetangaza kuwa, Samsung ndio brand ya kwanza inayoongoza kwa kunakiliwa kuliko brand nyingine.

Ripoti hiyo inadai kuwa kati ya makadirio ya nakala za simu janjaĀ 17,424,726 zilizo uzwa kwa mwaka 2017, asilimiaĀ 2.64% ya simu hizo zilikuwa zimenakiliwa au ni simu feki. Kampuni hiyo pia imetoa chati ya simu zilizoongoza kwa kunakiliwa na Samsung imeshika namba moja kwa kuongoza kwa zaidi ya asilimiaĀ 36.23% ya simu zote zilizo nakiliwa, huku simu zake za Samsung S7 zikiwa zinaongoza kwa kunakiliwa.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hata hivyo Apple nayo ilishika nafasi ya pili kwenye list hiyo kwa mwaka jana 2017 kwa kuwa na simu nyingi zilizo nakiliwa kwa kuchukua asilimia 7.72% ya simu zote zilizo nakiliwa, huku simu yaĀ iPhone 7 Plus ikiwa inaongoza kwa kunakiliwa zaidi. Simu nyingine zilizoongoza kwa kunakiliwa zaidi ni kama inavyo onyesha kwenye chati hapo chini.

Na hiyo ndio ripoti ya simu zilizo ongoza kwa kunakiliwa au kwa kuwa na simu feki zaidi na kama unavyoona kwenye list hapo juu Samsung imeshika kinara, hivyo ni vyema kuwa makini unapo nunua simu za samsung hasa simu za Samsung Galaxy S7.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Ripoti : Samsung Yaongoza Kwenye List ya Simu Zinazo Nakiliwa Zaidi
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment