Programu Mpya ya “Twitter Lite” Isiyotumia Kiasi Kikubwa cha Data

Sasa programu hii inapatikana rasmi Tanzania, download sasa
Programu ya Twitter lite Programu ya Twitter lite

Hivi karibuni Twitter imetangaza kuwa programu isiyotumia kiwango kikubwa cha data ya Twitter Lite imeanza kupatikana rasmi kwa watumiaji wa Android wa nchi zaidi ya 24 ikiwemo Tanzania.

Programu hii itakusaidia kuweza kutumia kiwango kidogo cha data huku ikiwa na uwezo wa kufunguka kwa haraka pamoja na kukupa muonekano ule ule wa programu ya kawaida uliyozoea ya Twitter.

Mbali na hayo Twitter imesema kuwa programu hiyo mpya ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwenye sehemu zenye uwezo mdogo wa internet ya 2G pamoja na 3G, Hata hivyo kwa mujibu wa twitter programu hiyo ya Twitter Lite kwa sasa imepunguzwa ukubwa na kufikia kiasi cha MB 3 hii itakuwa msaada mkubwa kwa watumiaji wenye simu zenye memory ndogo.

Advertisement

Programu ya Twitter Lite imetengazwa kuanza kupatika rasmi kwa nchi za Algeria, Bangladesh, Bolivia, Brazil, Chile, Colombia, Costa Rica, Ecuador, Egypt, Israel, Kazakhstan, Mexico, Malaysia, Nigeria, Nepal, Panama, Peru, Serbia, El Salvador, South Africa, Thailand, Tunisia, Tanzania pamoja na Venezuela.

Kama unatumia simu ya Android Unaweza kuanza kuitumia programu hiyo sasa, kwani kwa mtazamo wangu programu hiyo ni nzuri sana kwa simu zenye uwezo mdogo wa internet, inafunguka haraka sana ukilinganisha na programu ya kawaida ya Twitter, Unaweza kudownload kwa kubofya hapo chini.

Twitter Lite
Price: To be announced

Kwa watumiaji wa iOS mnaweza kutumia Twitter Lite kwa njia ya tovuti au kwa kupitia kisakuzi cha simu yako. Unaweza kufanya hivyo kwa kutembelea tovuti ya mobile.twitter.com/home kupitia browser ya simu yako.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use