Samsung Yagundua Teknolojia Mpya ya Kuchaji Battery kwa Dk 12

Battery zitakazo tengenezwa kwa teknolojia hiyo zitadumu na chaji zaidi
Kuchaji Battery Kuchaji Battery

Wataalamu kutoka kampuni ya Samsung Hapo jana wametangaza rasmi kuwa, wamegundua aina mpya ya teknolojia ambayo itawezesha kuchaji battery ya simu yako ya Samsung kwa muda wa dakika 17 pakee.

Wataalamu hao kutoka Samsung Advanced Institute of Technology (SAIT) wamesema kuwa,  teknolojia hiyo mpya inahusisha material za graphene ball technology ambazo zinauwezo mkubwa wa kujaa chaji haraka mara tano zaidi ya material ya lithium-ion ambayo ndio hutumika kutengeneza battery nyingi za simu na vifaa mbalimbali.

Kwa kuongezea kampuni hiyo imesema kuwa battery zitakzo tengenezwa na material hiyo zitakuwa na uwezo mkubwa wa kudumu na chaji kwani teknolojia hiyo inayo uwezo wa kuongeza hadi asilimia 45 ya nguvu za battery zinazotumika kwa sasa na Samsung.

Advertisement

Mbali na hayo kampuni hiyo imesema kuwa teknolojia hiyo pia inaweza kutumika kutengeneza battery za magari ya umeme kwani material ya graphene yanayo uwezo mkubwa sana wa kupitisha umeme kwa haraka ukitofautisha na material yanayo tengeneza battery za sasa ya Copper.

Bado haija julikana ni lini teknolojia hiyo ya graphene ball-based batteries ita anza kutumika lakini samsung kupitia tovuti yake ya habari imesema kuwa watumiaji wa simu za mkononi na magari ya umeme wategeme mabadiliko makubwa ya battery kwa miaka ya karibuni.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use