Jinsi ya Kubadili Simu Yoyote ya Android Kuwa Kama Galaxy S8

Sasa badili muonekana wa Simu yako ya Android kuwa kama S8
Samsung-Galaxy-S8 Samsung-Galaxy-S8

Kuna wakati unakuta umeichoka simu yako na mara nyingi hii inasababishwa na simu yako kuwa na muonekano wa aina moja, leo Tanzania Tech tutakupa maujanja ya jinsi ya kuipa simu yako muonekano mpya ambao utafanana kabisa na muonekano wa simu ya Samsung Galaxy S8.

Bila kupoteza muda twende tukajue mambo ya muhimu unayo hitaji ili kuweza kubadilisha muonekano wa simu yako kuwa kama wa simu ya Samsung Galaxy S8. Kwanza unatakiwa kuwa na bando angalau MB 200 au zaidi.

Kisha ingia kwenye soko la Play Store na Download programu hizi, unaweza kubofya hapo chini ili kupelekwa kwenye ukurasa maalumu wa programu hizo kwenye soko la Play Store.

Advertisement

  • S+ S8 Launcher
  • S8 Edge Mask
S8 Edge Mask
Price: Free
  • S8 Navigation bar

Baada ya kudownload programu hizo basi moja kwa moja fuata maelezo haya. Hatua ya kwanza fungua App ya S+ Launcher kisha bofya kitufe cha “GO” kisha bofya “OK” hapo utaona simu yako imebadilika na kuwa kama galaxy S8, lakini hatujaishia hapo..

Ukiwa hapo kwenye kioo mwanzo HOME bofya “S+ Settings” kisha shuka chini kidogo alafu bofya sehemu iliyo andikwa “Theme & UI & Icon Pack” baada ya hapo shuka chini kidogo kisha bofya “UI Size Mode” kisha chagua “Large Size” badili sehemu hii kulingana na ukubwa wa kioo chako.

Kisha sasa fungua App ya Edge Mask kisha bofya “Continue” kuendele kama litatokea tangazo bofya kitufe cha back kulifunga kisha chagua mahali palipo andikwa “Draw Permission” utaletewa ujumbe wenye sehemu mbili bofya “Allow” kisha shuka chini kidogo mahali palipo andikwa “Coners Color” kisha chakua rangi nyeusi, baada ya hapo shuka chini kidogo kisha chagua “Corners Size” kisha shikilia kwenye kitufe chenye rangi kisha sogeza mpka kwenye “19“.

Baada ya Hapo fungua App ya S8 Navigation kisha funga ujumbe unaotokea kwenye kioo chako kwa kubofya “OK” kisha bofya mahali palipo andikwa “Enable Navigation” kisha utatokea ujumbe ukitaka uwezeshe sehemu hii kwenye ya Accessibility. Bofya “OK” kisha shuka mwisho kabisa kisha bofya sehemu iliyo andikwa “S8 Navigation” kisha bofya kwenye kona kulia kuwasha sehemu hiyo.

Baada ya hapo utaona sehemu ya menu za chini ikiwa imewezeshwa kwenye simu yako, Muhimu kumbuka sehemu hii ni muhimu kama simu yako inavyo vitufe vya chini kwenye kioo na sio vilivyo jitenge nje ya kioo.

Baada ya Hapo shikilia kioo chako katikati zitatokea sehemu zingine nne bofya sehemu ya “Edit” kisha chagua Wallpaper kisha chagua s+ Color Wallpaper. Chagua rangi ya Wallpaper unayotaka kisha malizia kwa kubofya OK.

Na mpaka hapo utakuwa umepata muonekano wa Samsung Galaxy S8 kwenye simu yako ya kawaida ya Android…. Je unaonaje maujanja haya tuambie kwenye maoni hapo chini na kama kuna mahali umekwama usisite kutuandikia hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

4 comments
  1. Mi natumia sim ya Tecno Y6 lakini tatizi nikitaka dwnload S8 navigaction yakataa yataka niilipie App je nifanyaje nisilipie

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use