Kutana na ZTE Axon M Simu Mpya Yenye Vioo Viwili vya Kukunja

Huu ndio ulimwengu mpya wa teknolojia ya muundo wa Smartphone
ZTE AXON M ZTE AXON M

Pale linapokuja swala zima la muundo wa smartphone siku hizi karibia kila simu inakuja na muundo unaofanana pamoja na kioo kikubwa, lakini kwa namna ya tofauti kampuni ya ZTE imekuja na simu hii ya ZTE Axon M ambayo ina muundo wa tofauti na pengine huu ndio muundo wa simu za baadae.

Simu hii ambayo imezinduliwa hapo juzi inakuja na processor ya Snapdragon 821 chipset huku ikisaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani hadi GB 64 ambao unaweza kuongeza kwa kutumia Memory Card ya hadi GB 256.

Advertisement

Vioo vyote vya simu hii vimetengenezwa kwa teknolojia ya LCD uku vikiwa na uwezo wa hadi pixel 1080p, vioo hivyo vimeongezewa ulinzi na ugumu kwa kutumia Glass ya Gorilla Glass 5 huku vyote vikiwa na urefu wa inch 6.75 diagonally. Upande wa Battery simu hii inakuja na battery isiyotoka yenye uwezo wa 3180mAh.

Simu hiyo pia inakuja na mfumo wa undeshaji wa Android Nougat 7.1.2 na inategemewa kupata toleo jipya la Android 8 Oreo kwenye siku za mbeleni. Vilevile simu hii inakuja na Warrant ya miaka miwili popote pale utakapo kupitia programu ya kampuni hiyo ya Axon Passport M program.

Kwa upande wa bei simu hii inategemewa kutoka rasmi nchini marekani kupitia mtandao wa simu wa AT&T na itauzwa kwa dollar za marekani $725 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,650,000 kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Hayah! huo ndio ulimwengu mpya wa Smartphone niambie unaonaje hii ni simu ambayo ungependa kuwa nayo..? tuambie kwenye maoni hapo chini.. kama kawaida ili kupata habari za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store.

Chanzo : CNET

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use