Ukosefu wa 3G na 4G Kusababisha Ugumu wa Uchaguzi Kenya

Vituo vya Uchaguzi Kenya Kukosa Huduma Nzuri ya Simu
Uchaguzi Kenya 2017 Uchaguzi Kenya 2017

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, imetangaza kwamba robo ya vituo vyote vya kupigia kura nchini humo havina huduma nzuri ya mtandao wa simu wa 3G au ya 4G, imeripoti tovuti ya BBC.

Tume hiyo imesema maafisa wasimamizi wa uchaguzi katika vituo hivyo watalazimika kusongea hadi maeneo yenye huduma nzuri ya mtandao ndipo waweze kupeperusha matokeo.

Taarifa ya tume hiyo inasema kuna jumla ya vituo 11,155 ambavyo havina huduma nzuri ya mtandao ya 3G kati ya jumla ya vituo 40,883 kote nchini humo. “Maafisa wasimamizi wa uchaguzi watatafuta pahala penye huduma nzuri ya mtandao au watumie simu za setilaiti kupeperusha matokeo,” tume hiyo imeandika kwenye Twitter.

Advertisement

Vituo hivyo visivyo na huduma nzuri ya simu vinapatikana katika kaunti 45 kote nchini humo huku zikiacha kaunti za Nairobi na Mombasa pekee ambazo hazija kumbwa na tatizo hilo. Hata hivyo takwimu kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya zinaonesha maeneo mengi nje ya miji nchini humo hayana huduma ya 3G.

Ripoti kuhusu huduma ya simu na mtandao nchini Kenya ya mwaka jana inaonesha huduma ya 3G inapatikana katika asilimia 17 pekee ya ardhi ya Kenya. Hata hivyo, tofauti katika wingi wa watu maeneo mbalimbali, huduma hiyo huweza kufikia asilimia 78 ya wananchi nchini humo.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Kenya inasema kufikia wakati huo, kaunti ya Isiolo ndiyo pekee ambayo haikuwa na eneo hata moja ambalo lina huduma ya 3G. Hata hivyo ripoti hiyo inasema katika maeneo mengi, nchini kenya huduma inayopatikana ni ya 2G.

Hayo yakijiri, afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba pia amefafanua kwamba karatasi za kupigia kura zitahitajika kuwa na muhuri wa tume hiyo kabla ya mpiga kura kupiga kura.

Amesema karatasi ambazo zitapatikana ndani ya masanduku ya kura zikiwa hazina muhuri hazita hesabiwa kama kura halali. Marekebisho katika kanuni na sheria za uchaguzi yaliyofanywa mwaka huu yalikuwa yamefutilia mbali hitaji la kuwepo kwa muhuri katika karatasi za kura.

Hata hivyo, Bw Chiloba amesema tume hiyo imeamua kuwa karatasi za kura ni lazima zipigwe muhuri.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : BBC Swahili

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use