in

Premier League Imekaribia Tumia App Hizi Kuangalia Mpira Live

Premier League ni tarehe 11 mwezi huu, Jiweka karibu kwa app hizi

Premier-League

Msimu mpya wa ligi ya Premier umekaribia ili kujiweka karibu na mechi zote pamoja na matokeo kupitia simu yako ya mkononi nimekuwekea list ya app hizi bora ambazo zitakusaidia kupata matokeo pamoja na kuangalia mechi moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi.

Basi moja kwa moja bila kupoteza muda twende tukangalie app hizi, ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukusaidia kukaa karibu na mechi zote za ligi hiyo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Premier League – Official App Android

Premier League – Official App iOS

Hapa hakuna haja ya kusema maneno mengi kwani kwa kupitia app hii ambayo ni maalum kwa Premier League utaweza kupata habari zote kuhusu ligi hiyo ikiwa ni pamoja na matokeo, pamoja na mengine mengi, ukweli msimu huu ni vyema ukawa na app hii.

Sky Sports Live Football Score Centre Android

Sky Sports Scores
Price: To be announced

Kwa wapenzi wa mpira app hii ni muhimu sana kuwa nayo sio sababu ya Premier League pekee hapana bali app hii ni nzuri sana kama wewe unapenda michezo. Kwenye kipindi hiki cha msimu wa Premier League App hii uwa bora zaidi kwani habari zote na matokeo ya moja kwa moja utayapata kupitia App hi.

BBC Sport

Hii ni app nyingine yenye uwezo mkubwa wa kukupa habari na matukio ya Live kabisa ya ligi ya Premier League, kupitia app hii utapata habari zote mpya na ambazo zinatokea hapo hapo uwanjani kifupi app hii ni muhimu sana kuwa nayo msimu huu.

365Scores – Sports Scores Live

Kama uko bize sana hasa siku za wikina ungependa kupata taarifa pindi tu goli litakapo fungwa, pamoja na pindi mechi itakapo anza basi app hii ni muhimu sana kuwa nayo msimu huu. App hii ni moja ya app inayotegemewa sana kwenye swala la kutoa matokeo ya mpira wa miguu moja kwa moja pindi pale yatakapo tokeo kwenye viwanja. Jaribu uonee…!

theScore – Sports News & Scores: Football & More

Kama unataka habari pamoja na matokeo ya mechi mbalimbali basi download app hii utaipenda, App hii inasifika sana kwa sasa na ni moja kati ya app bora sana kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu.

Na hizo ndio baadhi ya app ambazo ukiwa nazo msimu huu wa ligi ya Premier League, unaweza kuangalia programu zingine za kuangalia michezo mbalimbali kwa kusoma makala hii hapa. Kama una maoni au kama unajua kuna app inayo fanya vizuri msimu huu wa Premier League tuambie hapo chini kwenye maoni nasi tutaongeza kwenye list hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Premier League Imekaribia Tumia App Hizi Kuangalia Mpira Live
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments