in

Vitu Ulivyokua Hujui Kuhusu Dubai Kwa Upande wa Teknolojia

Je unajua haya kuhusu Dubai kwa upande wa teknolojia

Robocop_Dubai

Leo ngoja angalau tuangalie kidogo kwa upana kuhusu nchi ya dubai, dubai ni moja kati ya nchi tajiri sana duniani na ni moja kati ya nchi inayo-kuwa kwa haraka sana kutokana na utajiri wake wa kuwa na mafuta pamoja rasili mali zingine. Lakini leo ngoja tuangalie nchi hii kwa upande wetu yaani teknolojia, katika kuangalia huku haya ndio mambo ambayo nimekuandalia kwa siku ya leo.

  • Polisi Roboti Kwenye Miji ya Nchi ya Dubai

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Polisi hawa ni polisi ambao wanategemewa kuanza kulinda nchi ya dubai kwenye miaka ya karibuni, roboti hawa ambao wana urefu wa futi 5 pamoja na uzito wa kilogram 100kg wame -tengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu yenye uwezo wa kusoma tabia ya mtu kwa kuangali sura (facial expressions) ikiwa pamoja na sensor mbalimbali na kamera zenye uwezo wa kutuma picha na video kwenda makao makuu ya polisi huku nchini dubai.

  • Magari Yaliyotengenezwa Kwa Gold

Magari haya ni moja kati ya magari ambayo unaweza kuyaona pekee kwenye miji ya nchi ya dubai, magari haya mara nyingi huwa ni magari ya watoto wa matajiri au matajiri wenyewe wenye visima vya mafuta nchini humo. Kwa upande wa magari hayo huwa yana-tengenezwa na kupakwa gold ambayo upakwa kwa kiasi kikubwa sana karibia asilimia 85 ya rangi ya gari hilo.

  • Magari ya Kifahari ya Polisi

Kama ulidhani kuwa magari ya polisi ni lazima kuwa magumu yaliyochoka yenye uwezo wa kupita sehemu yoyote basi jiulize tena maana nchini dubai magari ya polisi ni ya kifahari kuliko magari mengine ambayo hata watu wanaendesha nchini humo. Jeshi la polisi la nchi hiyo lina magari kama bugati, lamborghini pamoja na magari mengine ya kifahari sana.

  • Taxi Ambazo ni Drone

Kama wewe ni moja wa watu ambao wangependa kupanda taxi za drone basi dubai ndio nchi ya kwenda kwa sasa, drone hizi zinategemewa kuwa moja kati ya usafiri wa kuchagua nchini dubai kwenye miaka ya karibuni. Drone hizo zinauwezo wa kubeba mtu mmoja na zinaongozwa kwa kutumia mfumo wa ramani.

  • ATM zenye Uwezo wa Kutoa (Kununua) Gold

Kama unataka kununua Gold basi hii ndio njia mpya ya kufanya hivyo nchini dubai, wakati teknolojia hii ikiwa ni teknolojia ya mda kidogo bado imekua ni moja kati ya vitu vya kushangaza kidogo pengine kutokana na ustarabu wa nchi kama dubai na nyingine ambazo kwa sasa zinatumia mfumo huu wa kuuza Gold kuptia ATM. Mashine hii inauza gold ndogo ndogo ambazo ziko kwenye paketi nzuri ndogo ambapo unaweza kulipia kwa pesa cash pamoja na kadi ya bank.

  • Tattoo za Gold Mwilini

Dubai ndio kisiwa cha gold lakini hii ndio iliyovunja rekodi kwa upande wangu, kuwa na tattoo ya gold ni kitu cha kawaida sana kwa nchi hiyo na kama ulikua unajiuliza tattoo hiyo haikai muda mrefu lakini unaweza kuiondoa na kurudisha hapo baadae kama utakuwa unataka… Unaweza kuona sio teknolojia lakini nimeshindwa kuvumilia imenibidi niku-fahamishe tu! kuhusu hili..mhh

Na hivyo ndio baadhi ya vitu ambayo nimekuandalia leo kuhusu teknolojia kwa upande wa nchi ya dubai, kama unajua vingine kuhusu teknolojia kwa nchi ya dubai usiache kutuandikia kupitia maoni hapo chini nasi tutaendelea kuongeza makala hii kila tutakapo pata vitu vipya hivyo usikae mbali….

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Vitu Ulivyokua Hujui Kuhusu Dubai Kwa Upande wa Teknolojia
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.