in

Samsung Kufidia Wateja Watakao Endelea Kutumia Simu za Samsung

Wateja wa Samsung kuanza kulipwa fidia baada ya matatizo ya simu za Samsung Galaxy Note 7

fidia

Kampuni ya teknolojia ya samsung imetangaza rasmi hapo jana kuanza kuwalipa fidia wateja wake ambao wataendelea kutumia simu kutoka kampuni hiyo baada ya kurudisha simu za Galaxy Note 7 ambazo zimesitishwa matumizi yake.

Samsung imetoa taarifa za kuhimiza wateja wake kurudisha simu hizo kwenye maduka ambayo wamenunua ili kubadilishiwa simu hizo au kurudishiwa hela, hata hivyo kampuni ya Samsung ilitangaza kuwa inatoa zawadi kwa wateja wake ambao wata chagua kuendelea kutumia simu za samsung baada ya kurudisha simu hizo za Galaxy Note 7, hata hivyo wateja wa Korea Kusini wamepewa fursa na Samsung ya kubadilishiwa simu hizo kwa simu nyingine kama vile Apple iPhone 7, LG G5, LG V20, Galaxy S7, Galaxy S7 Edge au Galaxy Note 5.

Kuhusu fidia hiyo Samsung ilisema kuwa inatoa fidia ya fedha taslim kiasi cha dollar za marekani $100 kwa wateja wake ambao wataendelea kutumia simu kutoka kwenye kampuni hiyo yani Galaxy S7, Galaxy S7 Edge au Galaxy Note 5. Hata hivyo Samsung imetangaza wataje wake kuhakikisha wanarudisha simu hizo za Galaxy Note 7 hadi ifikiapo tarehe 30 Novemba Mwaka huu.

Ili kujua Samsung imepanga kuja na kitu gani tena ili kurudisha tena uaminifu kwa wateja wake endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.