Samsung Galaxy Note 7 Kurudi Sokoni September 28

Baada ya Misikusuko ya Sasa Samsung imetangaza Kurudi sokoni Mwezi September Mwaka Huu
samsung-galaxy-note-7 samsung-galaxy-note-7

Habari njema kwa wapenzi wa Samsung Galaxy Note 7 baada ya simu hizo kuonekana kusumbua kwa muda hadi kusababisha Samsung kuzuia usafirishaji wa simu hizo, sasa wapenzi wa simu hizo wakae tayari kununua tena simu hizo zisizokua na matatizo yoyote, mauzo hayo pamoja na usafirishaji wa simu hizo utaanza rasmi kuanzia siku ya tarehe 28 mwezi huu yani september.

Habari zilizotangazwa na kituo cha utangazaji cha CNN Money zinasema kuwa mauzo hayo yataanza rasmi korea kusini na baadae kwenda kwenye nchi zingine pale hali itakapo ruhusu. Samsung hivi karibuni ilipata hasara kubwa baada ya taarifa kutoka nchi mbalimbali kuhusu simu hizo mpya za Samsung Galaxy Note 7 kulipuka kiasi cha kampuni hiyo kutangaza kusitisha matumizi ya simu hizo mpaka hapo itakapo tangaza.

Kama unataka kujua mauzo ya simu hizo za Note 7 yataanza lini hapa Tanzania pamoja na Afrika Mashariki kwa ujumla endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use